Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk
Suleiman (kushoto) . akifafanua jambo kuhusu filamu ya MV spice
Islander. Kulia ni Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce
Fissoo. 
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo(kulia) akifafanua jambo kuhusu
filamu ya MV spice Islander . Kushoto ni Katibu Mtendaji wa Bodi
ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman .
Katibu Mtendaji
wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo(kushoto) akipeana mkono na
Mwakilishi wa kampuni ya kutengeneza filamu ya Steps, Moses Mwanyilo
(kulia).Katibu Mtendaji wa Bodi ya Sensa ya Filamu ya Zanzibar,
Suleiman Mbarouk Suleiman (kushoto) akipeana mkono kulia Mwakilishi wa
kampuni ya kutengeneza filamu ya Steps, Moses Mwanyilo.
(Picha na Magreth Kinabo)
Viongozi
wa Bodi za Filamu wa Tanzania Bara na Zanzibar wametoa ushauri kwa
wasanii nchini kuacha kutumia majanga halisi kwa ajili ya kutengenezea
filamu Kibiashara.
Kauli
hiyo imetolewa jana na viongozi hao , wakati wa kikao cha kati ya
Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Joyce Fissoo na Bodi ya
Sensa ya Filamu ya Zanzibar, Suleiman Mbarouk Suleiman na Mwakilishi
wa kampuni ya kutengeneza filamu ya Steps, Moses Mwanyilo
kilichofanyika jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika kikao hicho, Bi.Fissoo alisema kampuni hiyo imetengeneza
filamu ya MV Spice Islander kwa kuchukua picha halisi za ajali ya
MV spice,ambayo iliwasilishwa katika ofisi yake Novemba 2013 kitendo
ambacho ni kinyume na sheria , taratibu na kanuni za utengenezaji wa
filamu.
Alisema
filamu hiyo ilichukua picha halisi ya ajali hiyo, hivyo ofisi yake
ilimwandikia barua mtengenezaji huyo kuwa ibadilishwe, lakini aliomba
ashiriki kikao na bodi. Hata hivyo aliitwa mara nne kwa ajili ya kikao
na bodi hiyo lakini hakushiriki badala yake alileta marekebisho ya
filamu hiyo mara tano ambayo bado yalikuwa na kasoro hizo.
Naye
Bw. Suleiman alisema filamu hiyo ni muhimu . Hivyo alimtaka
mtengenezaji huyo kutoingilia uhuru wa mtu, jamii na Serikali na kutaka
filamu hiyo ifanyiwe marekebisho, hivyo ni vema wasanii wakawa wabunifu
kutengeneza filamu zinazogusa bila kutumia uhalisia wa janga na
majina halisi.
Aliipongeza
bodi ya filamu ya Bara kwa ushirikiano waliouonesha kwa kuwa filamu
ikataliwa Zanzibar na Bara inakataliwa kwani kazi kama hiyo
iliwasilishwa Zanzibar na ilikataliwa kwa kuwa ajali iliyotokea si
sherehe, bali itatonesha vidonda vya watu walioathirika.
Kwa upande wake mwakilishi wa kampuni hiyo alikiri kosa hilo na aliahidi kufanya marekebisho katika filamu hiyo.
Na ZanziNews