Katika mwaka wa 1962 Nelson
Mandela aliondoka Afrika kusini kisirisiri na kwa muda wa miezi saba
alikuwa akitembelea mataifa mengi ya bara la Afrika.
Chama cha African National Congress, ambacho
kilikuwa ndio kimepigwa marufuku na utawala wa ubaguzi, kilikuwa
kimeanzisha mapambano ya kijeshi kupitia jeshi lake la Umkhonto we
Sizwe.Kazi ya mandela ilikuwa ni kutafuta uungwaji mkono wa hali na mali kutoka mataifa mengine ya Afrika na pia kutafuta mataifa yaliyo tayari kuwapa mafunzo ya kijeshi makurutu wake akiwemo yeye mwenyewe.
Alipata mafunzo ya kijeshi nchini Morocco, kutoka kwa wanajeshi wa Algeria waliokuwa wanatumia ardhi ya Morocco kama kituo chao kupigana dhidi ya utawala wa kikoloni wa Ufaransa.Mafunzo mengine yalifanyika Ethiopia.
Katika kuangalia safari ya maisha ya Nelson Mandela zipo taarifa kwamba kabla ya kufungwa jela, Marehemu Nelson Mandela aliwahi kuishi nchini Tanzania katika familia moja ambapo wakati anaondoka aliacha baadhi ya vitu, vikiwemo viatu .
John Solombi aliitembelea familia hiyo iliopo Kilimanjaro kaskazini mwa Tanzania na kutuandalia taarifa ifuatayo.