Rais Jakaya Mrisho Kikwete leo ameongoza maadhimisho ya miaka 52 ya uhuru wa Tanganyika uliopatikana Desemba 9, 1961.
Miaka 52 imetimia tangu Tanganyika (sasa Tanzania), kupata uhuru wake kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza, Desemba 9, mwaka 1961.
Maadhimisho
haya yamefanyika uwanja wa uhuru hapa Dar es salaam,Rais Jakaya Kikwete
amekagua gwaride la vikosi mbalimbali vya ulinzi na usalama ambavyo pia
vimetoa heshima kwa kiongozi huyo kwa mwendo wa pole na haraka.kikosi
cha anga pia kimetoa heshima zake na burudani mbalimbali ikiwamo ngoma
na michezo ya halaiki. Sherehe hizi zimehudhuriwa na wageni mbalimbali
waalikwa wa ndani na nje ya nchi, wakiwamo mabalozi wanaoziwakilisha
nchi zao hapa nchini.
Katika
maadhimisho haya kwa mwaka jana, yaliyohudhuriwa na viongozi 14 wa
kutoka Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC), Rais
Kikwete aliwataka Watanzania kujivunia na kuyaenzi mafanikio ya kisiasa,
kiuchumi na kijamii yaliyopatika tangu nchi ilipopata uhuru.