Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimshukuru Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, baada ya kukabidhiwa hundi ya shilingi milioni 100 kutoka benki hiyo kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo katika Mkoa wa Morogoro, mwezi uliopita katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam Jana February 4, 2014 na kuhudhuriwa pia na Mhesimiwa William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia pia masuala ya maafa pamoja na maafisa wa CRDB.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, baada ya kukabidhiwa
hundi ya shilingi milioni 100 kutoka benki hiyo kusaidia waathirika wa
mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo katika
Mkoa wa Morogoro, mwezi uliopita katika shughuli fupi iliyofanyika
Ikulu, Dar Es Salaam Jana February 4, 2014 na kuhudhuriwa pia na
Mhesimiwa William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia pia masuala ya maafa pamoja na maafisa wa CRDB.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete Mhesimiwa akimkabidhi Mhe William
Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia pia masuala
ya maafa pamoja na maafisa wa CRDB, hundi ya shilingi milioni 100
iliyotolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei,
zikiwa ni msaada wa benki hiyo kwa waathirika wa mafuriko yaliyozikumba
wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo katika Mkoa wa Morogoro, mwezi
uliopita katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam Jana
February 4, 2014.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dkt. Charles Kimei, baada ya kukabidhiwa
hundi ya shilingi milioni 100 kutoka benki hiyo kusaidia waathirika wa
mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero na Gairo katika
Mkoa wa Morogoro, mwezi uliopita katika shughuli fupi iliyofanyika
Ikulu, Dar Es Salaam Jana February 4, 2014 na kuhudhuriwa pia na
Mhesimiwa William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia pia masuala ya maafa pamoja na maafisa wa CRDB. (Picha na Ikulu)
TAARIFA
KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jana,
Jumanne, Februari 4, 2014, amepokea hundi ya Sh. milioni 100 kutoka Benki ya
CRDB kusaidia wahanga wa mafuriko yaliyozikumba wilaya tatu za Kilosa, Mvomero
na Gairo katika Mkoa wa Morogoro, mwezi uliopita.
Rais
Kikwete amekabidhiwa hundi hiyo na Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dkt. Charles
Kimei katika shughuli fupi iliyofanyika Ikulu, Dar Es Salaam, na kuhudhuriwa
pia na Mhesimiwa William Lukuvi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu
anayeshughulikia pia masuala ya maafa.
Akizungumza
kabla ya kukabidhi hundi hiyo kwa Rais Kikwete, Dkt. Kimei amesema kuwa fedha
hizo ni sehemu ya Sh. Milioni 850 ambayo ni asilimia moja ya faida ya Benki
hiyo ambayo hutengwa kila mwaka kwa ajili ya kuunga mkono shughuli za jamii.
“Sote tumeona madhara makubwa yaliyosababishwa na mafuriko haya. Watu wengine wamepata hasara – akinamama, watoto, wajawazito na wazee. Hawa wote wanahitaji misaada ya ziada ili kukabiliana na athari za mafuriko hayo,” amesema Dkt. Kimei.Akizungumza kabla ya kupokea hundi hiyo, Rais Kikwete ameelezea kwa ufupi mafuriko hayo yaliyotokea alfajiri ya Januari 22, mwaka huu, 2014 na athari ambazo zimetokana na mafuriko hiyo katika maeneo ya Magole, Dakawa na Mateteni huko Dumila, Wilaya ya Mvomero, ambayo aliyatembelea mwishoni mwa mwezi uliopita kujionea madhara.
“Waswahili husema kuwa ajali haina kinga na ni kweli. Unajua mafuriko yaliyotokea katika eneo la Dumila hayakutokana na wala na mvua ya pale. Mvua ilinyesha kule Kiteto, Mkoa wa Manyara, lakini walioathirika kwa mafuriko ni hawa jamaa zetu wa Dumila. Bahati tu ni kwamba mafuriko hayo yalilikumba eneo hilo alfajiri wakati watu tayari wameamka na ndio maana hakuna mtu aliyepoteza maisha yake katika eneo hilo,” amesema Rais Kikwete na kuongeza:
Akizungumza katika shughuli hiyo, Mheshimiwa Lukuvi amesema kuwa tathmini mpya imeonyesha kuwa watu walioathirika katika mafuriko hayo ni 9,268 na kati ya watu hao kaya 522 hazina makazi kabisa baada ya nyumba zao kubomolewa na maji, nyingi zaidi 466, zikiwa katika Wilaya ya Kilosa.Amesema kuwa nyumba 537 zimeharibika hata kama wenye nyumba hizo bado wanaendelea kuishi ndani ya nyumba hizo na nyingine 1,036 ziliingiwa na maji hata kama hazikuharibika.“Watu wamepata hasara kubwa. Baadhi nyumba zao zimesombwa na kuzolewa na maji, nyingine zimebomoka, watu wamepoteza mali zao nyingi kama vile nguo na wengine hata chakula chao kimesombwa na maji. Wanahitaji msaada na kwa kweli sisi katika Serikali tunaishukuru sana CRDB kwa kutoa msaada huu kwa sabababu unachangia katika jitihada za Serikali kukabiliana na tatizo hili.”
Imetolewa
na:
Kurugenzi ya
Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR
ES SALAAM.