Maelfu ya watu wanaendelea
kuwasili katika uwanja mkubwa wa FNB mjini Johanessburg kwa kuhudhuria
misa ya wafu ya hayati Nelson Mandela,
Rais wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa
Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon watakuwa miongoni mwa viongozi wa dunia
watakaohudhuria misa hiyo.Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani.
Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu.
Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini.
na BBCSwahili