MADEREVA WAPATIWA KOZI FUPI




MADEREVA wa naoendesha magari ya abiria wamepatiwa mafunzo rasmi ili kupunguza ajali zitokanazo na kutojiamini.

Mafunzo hayo yameendeshwa na Chuo cha VETA mkoa wa Mbeya ambayo hutolewa kwa muda mfupi ili kupambana na ajali zitokanazo na madereva ambao wengi kukosa kujiamini.

Akizungumza katika sherehe za kuhitimisha mafunzo hayo Makamu mkuu wa Chuo cha VETA mkoa wa Mbeya Timale Kaloli, amesema wanaendesha mafunzo hayo ya muda mfupi ili kuwaimarisha madereva na kupunguza ajali.

Alisema ajali nyingi zinazotokea alilimia kuwa husababishwa na madereva wale ambao bado hawajapatiwa mafunzo hayo rasmi.

Veta ilianza kuendesha mafunzo hayo ya wiki mbili tangu mwezi Mei mwaka jana ambapo hawa wa sasa walianza mwezi Disemba na kumaliza mafunzo mwezi Januari na mpaka sasa wamefundisha madereva 931 ambao wamepata mafunzo hayo rasmi.

Kaloli alisema madereva wamepatiwa elimu ya huduma ya Kwanza, Udereva salama na kujihami, kubadilishwa tabia na Suala la zima la kukomesha ajali zinazo zuilika.

Aliitaka serikali katika suala zima la kupunguza ajali hapa nchini iwazuie madereva kufanyakazi hadi wapatiwe mafunzo hayo rasmi ndipo waenderee na udereva.

Katika mafunzo hayo Veta imekua ikikabiliwa na changamoto nyingi ikiwemo ya kuchelewa kupitishwa fomu za kubadilishiwa leseni kwa wahitimu wa kozi hiyo baada ya kupewa cheti cha kuhitimu.

Wahitimu waliohitimu sasa ni wa madaraja tofauti tofauti ambayo yamepangwa C, C1, C2, na C3 kwa mujibu wa utaratibu mpya wa leseni za madereva wabebao abiria.

Kaloli aliitaja kaulimbiu ya Veta Mbeya kuwa ni ‘pata mafunzo ili kuepusha ajari’ na kuongeza kuwa madereva ni muhimu wakapata kozi hiyo

Related Posts