Kati ya wachezaji wanaotawala sana vichwa vya habari hivi sasa ni Alexis Sanchez, kuna habari zinasema kwamba mwisho wake kuichezea Arsenal umekaribia lakini kuna habari zinazosema anabaki Arsenal.
Kwa sasa Sanchez yupo katika majukumu ya timu yake ya taifa na mambo mengi ambayo yanazungumzwa kuhusu yeye sio ya kuaminika kwa kuwa mwenyewe Sanchez hajasema lolote amekaa tu kimya.
Lakini baada ya ukimya wa muda mrefu Sanchez ameibuka na kusema kitu kuhusiana na suala lake la usajili, Alexis Sanchez hajaongea kile ambacho mashabiki wanataka kusikia kwani ameongea kwa lugha ya mafumbo.
“Naangalia ambacho wakala wangu atakifanya, ila kwa sasa kitu pekee katika kichwa changu ni kuisaidia Chile katika michezo iliyoko mbele yetu, wawawkilishi wangu wanafanya vitu kwa ajili yangu na watakaa na klabu kujua nini ni bora kwa ajili yangu” alisema Sanchez.
Tayari tetesi zilisema Alexis Sanchez anakaribia kumwaga wino katika klabu ya Manchester City lakini kumejitokeza wapinzani wapya wa Man City ambao ni klabu ya Bayern Munich wanaotajwa kumtaka Sanchez kwa nguvu zote.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!
from Blogger http://ift.tt/2sKClaw
via IFTTT