“Fair play” ndio kitu ambacho kimekuwa kikisisitizwa na Fifa kila siku, mpira unatakiwa utumike kama sehemu ya kuleta amani kati yetu,upendo kati yetu na pia kuwafariji wale waliopoteza faraja za maisha.
Lakini Saudi Arabia kwao ilikuwa tofauti wakati wa mchezo kati ya Saudi Arabia dhidi ya Australia, katika mchezo huo wachezaji walipaswa kujipanga mstari kabla ya mchezo huo kama kumbukumbu na pole kwa wahanga wa tukio la kigaidi lililotokea mjini London.
Australia walishikana mabega na wakajipanga mstari lakini wachezaji wa kikosi cha kwanza wa Saudi Arabia hawakufanya hivyo kwani kila mmoja alikaa kivyake akifanya yake na huku baadhi ya watu wa benchi lao la ufundi walionekana wakiwa wamekaa wakati wa tukio hilo.
Japokuwa kiongozi mmoja wa chama cha soka nchini Saudi Arabia amedai kwamba kwao utaratibu wa kupanga mstari huwa haupo lakini kumbukumbu zinaonesha kwamba mwaka 2005 timu hiyo ya taifa ya Saudi Arabia ilishawahi kupanga msatari kwa ajili ya “moment of silence”.
Chama cha soka cha Saudi Arabia kimeomba radhi kwa wahanga wa tukio hilo na kimesisitiza kwamba kinapinga kwa nguvu zote masuala ya kigaidi na tukio walilofanya halikuwa na nia ya kuwaudhi wahanga wa tukio lililotokea London.
Katika tukio hilo la kigaidi lililotokea London kulikwa na Waaustralia wawili waliofariki Sara Zelenak na Kirsty Boden walifariki katika mlipuko huo na Sara alikuwa ni nesi alifariki wakati akikimbia kwenda kujaribu kumuokoa mgonjwa.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!
from Blogger http://ift.tt/2t26JfV
via IFTTT