MAOMBI YASHUGHULIKIWE ELIMU IBORESHWE



SERIKALI imeombwa kuboresha mazingira ya kufundishia na kutekeleza maombi yanoyokuwa yanatolewa na walimu wakuu mbalimbali ili kuweza kuboresha elimu hapa nchini.
 
Hayo yalibainishwa na mwalimu mkuu wa shule ya msingi Uhuru, Bi Zenobia Kapere iliyopo jijini hapa, alisema serikali inatakiwa iyatekeleze kwa wakati maombi yatolewayo na walimu wakuu wa shule ili elimu ya hapa nchini iboreke.

Bi Kapere alisema kuwa shule yake imekuwa ikikabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya upungufu wa vitabu na vifaa vya kufundishia pamoja na vyumba vya madarasa.

Aitha ameongeza kuwa wananchi wamefanikisha kujenga vyumba viwili vya madarasa na kuomba uongozi wa jiji la Mbeya uweze kumalizia ukarabati wa vyumba hivyo ili viweze kutumiwa na wanafuzi.

Sanjali na hayo amesema kuwa shule hiyo ina upungufu wa madarasa na ukizingatia ina wanafunzi zaidi ya elfu moja na vyumba vilivyopo ni 12 tu jambo ambalo linapelekea msongamano wa wanafuni darasani.

Mbali na hayo ametoa wito kwa jamii kuwa hawatakiwi kukata tamaa katika suala la ujenzi wa madarasa na kuongeza kwamba kwa kufanya hivyo kutasaidia kuinua kiwango cha elimu.

Alisema akielimishwa mtoto atakuja kukusaidia menyewe mzazi na zio mwalimu hivyo ni vyemba kama wazazi watajitoa ili kuhakikisha wana funzi wanasomea katika mazingira mazuri.

Mtoto hufauru kama atasomea mahali pazuri na kwa muda wa asubuhi kuliko kuingia mchana kama zinavyo fanya shule zingine ambazo hazina nadarasa ya kutoha.