WATU wawili wamefariki dunia mkoani Mbeya ka matukio mawili tofauti likiwemo la mtu mmoja aliyefahamika kwa jina la John Ndelwa kazi wa chemu chemu uyole mwenye umri wa miaka 27 aliuwawa kwa kupigwa na kitu butu sehemu ya kichwa chake .
Kamanda wa Polisi mkoa wa mbeya Bw Advocate Nyombi amesema tukio la kwanza lilitokea juzi majira ya saa 1:00 za usiku katika eneo la chemu chemu uyole na amesema kuwa mbinu ilyotumika ni kumpigia simu marehemu akiwa nyumbani kwake na alipotoka nje aliuwawa hapo papo.
Nyombi alisema mtuhumiwa mmoja aliyehusika na tukio hilo anayefahamika kwa jina la Vasco Lwenje mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa wa songwe amekamatwa na simu ya marehemu na amekiri kuwa anahusika na tukio hilo.
Aidha alisema mtuhumiwa yupo mahabusu na mwili wa marehemu umehifadhiwa katika hospitali ya rufaa mbeya na upelelezi unaendelea.
Nyombi alisema tukio la pili lilitokea majira ya saa 2:00 eneo la songwe Mbeya vijijini gari lenye namba za usajili T. 155 BER scania basi la kampuni ya ilasi likiendeshw na dereva aitwae Brown Msaka mwenye umri wa miaka 44 mkazi wa Dar es salaamu likiwa limetokea Dar es salaamu kuelekea Tunduma lilisababisha kifo cha Laitoni Mwaluanda mwenye umri wa miaka 28 mkazi wa songwe na kusababisha kifo chake papo hapo .
Kamanda Nyombi alisema chanzo cha ajali ni mwendo kasi wa gari na dereva amekamatwa yupo kituo cha polisi songwe.
Aliongeza kuwa hatua za kisheria zitachukiliwa ili dereva huyo afikishwe mahakamani na mwili wa marehemu umehifadhiwa hospitali teule ya ifisi