Kwa hali hii kuna usalama na mtu kupona kweli?.
Wanafunzi 60 wa jinsi ya Kiume wa Shule ya Sekondari Simbega Kata ya Iyula, Wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya wamenusurika kifo baada ya lori walilokuwa wakisafiria, kutoka Kijiji cha Ruanda wilayani humo kuacha njia na kisha kupinduka.
Ajali hiyo imeyokea mita chache baada ya kupanda lori hilo, ambapo, wanafunzi wenzao wa jinsi ya kike kutangulia na lori jingine wakitokea mchezoni baada ya dereva wa lori hilo Bwana Juhudi Shonde kushindwa kulimudu gari hilo wakati likipanda mlima ndipo alipoamua kuruka na kuliacha gari hilo likirudi nyumba na kisha kupinduka likiwa na wanafunzi ndani.
Tukio hilo limetokea majira ya saa 3 usiku Februari 16, ambapo kati ya wanafunzi 60 waliokuwemo 37 na mwalimu mmoja wamejeruhiwa na kukimbizwa katika Hospitali ya Serikali Mbozi na wanafunzi wanane na mwalimu mmoja wamelazwa katika Hospitali ya Ifisi, Wilaya ya Mbeya Vijijini.
Miongoni mwa majeruhi waliolazwa katika Hospitali ya Mbozi wawili hali zao ni mbaya kutokana na kuvunjika miguu na Daktari wa zamu aliowapokea amewataja kuwa ni pamoja na Bahati Mwashambwa na Ajuaye Shonde na wliopo Hospitali ya Ifisi ni Mwalimu Enock Mabula ambaye ameumia goti na kupata majeraha.
Kwa upande wake Mkuu wa Shule hiyo Bwana Jacob Nsenye, amesema wazazi wa wanafunzi hao wasiwe na hofu hali zao zinaendelea vema kwa mujibu wa daktari.