Baada ya msimu kumalizika kocha wa Chelsea Antonio Conte aliamua kuongea na wachezaji wake kupitia ujumbe mfupi wa message ambapo aliwapongeza kuhusu msimu uliopita na kuwaambia matarajio yake juu yao kuhusu msimu ujao wa ligi kuu ya Epl.
Chanzo kimoja cha habari kimedai Antonio Conte hakumtumia Costa message mbaya lakini alimuambia maoni yake kama kocha lakini Mhispania huyo hakupendezwa na maoni ya Conte hivyo akamjibu Conte vibaya na ndipo Muitaliano huyo alipokasirika na kumuambia Costa kuwa hamtaki katika kikosi chake.
Costa kuona amejibiwa vibaya na Conte naye akaanza kumjibu vibaya hali iliyopelekea wawili hao kutumiana message mbovu na baadae Diego Costa alikasirika sana akaamua kutuma message hizo kwa wachezaji wote wa Chelsea aliokuwa na namba zao.
Tayari mgogoro huo umechukua sura mpya kwani mmiliki wa klabu ya Chelsea tajiri Roman Abromovich amechagua upande wake katika pande hizo mbili zinazovutana na Roman anaona hakuna mchezaji mkubwa kuliko kocha hivyo na yeye yuko upande wa kocha wao.
Chelsea wanapambana kutafuta mshambuliaji namba 9 ambaye anaweza kuziba nafasi ya Diego Costa na ugomvi kati ya Costa na Conte umezidi kuisukuma Chelsea kutafuta saini ya mchezaji wao wa zamani Romelu Lukaku ambaye thamani yake inatajwa kuwa euro 100m.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!
from Blogger http://ift.tt/2smd2OF
via IFTTT