Showing posts with label Umoja wa Ulaya. Show all posts
Showing posts with label Umoja wa Ulaya. Show all posts
Magari kumi maarufu duniani

Magari kumi maarufu duniani

The World Car of the Year awards will be handed out at the New York motor show on March 28. In order to determine a winner, a 66-strong panel of motoring journalists from around the world have agreed on what they regard as the 10 best new cars of the last 12 months. Click through this gallery to see their choices, as well as what we awarded each car when we tested it. Do you agree? 
Audi A3
Bei:£19,205 


Range Rover review
Land Rover Range Rover
Bei: £71,295

Mazda6 review
Mazda6
Bei: from £19,595

Mazda CX-5 review - May 5, 2012
Mazda CX-5
Bei: £21,395
Mercedes-Benz A-class review
Mercedes-Benz A-class
Bei: from £19,000
  
Peugeot 208 driving
Peugeot 208
Bei:  £9,995

Porsche Boxster review
Porsche Boxster/Cayman
Price: from £37,589

The world's best performance cars
Subaru BRZ/Toyota GT86
Bei:  £24,995
Volkswagen Golf review
Volkswagen Golf
Bei: from £16,285

Volvo V40 review
Volvo V40
Price: from £19,745
 Waziri mkuu wa Ukraine ajiuzulu

Waziri mkuu wa Ukraine ajiuzulu


Maandamano nchini Ukraine
Rais wa Ukraine, Viktor Yanu-kovich, amekubali ombi la kujiuzulu kwa waziri mkuu wa taifa hilo, Mykola Azrov, pamoja na baraza zima la mawaziri licha ya hatua muhimu kupigwa mnamo Jumanne.
Hata hivyo mawaziri hao waliojiuzulu wanasalia kuwa wasimamizi wa wizara zao hadi pale serikali mpya itakapo buniwa.
Awali bunge la Ukrain lilipiga kura ya kuifutilia mbali sheria kali dhidi ya maandamano ambayo ilizua ghasia tangu iidhinishwe mwezi uliopita.
Kura ya kuifutilia mbali sheria hio ilipigwa na asilimia kubwa ya wabunge wa taifa hilo. Sheria hio ilipiga marufuku waandamanaji kutumia majengo ya umma pamoja na kuvaa vinyago.
Mwandishi wa BBC nchini Ukraine, amesema kuwa upinzani utaiona hatua ya waziri mkuu kujiuzulu pamoja na kufutilia mbali sheria inayozuia maandamano kama ushindi kwao
Mgogoro wa kisiasa nchini Ukraine, ulianza kama maandamano ya amani mwezi Novemba wakati ambapo Rais Yanukovych alipokataa kutimiza ahadi yake ya kushirikiana na Muungano wa Ulaya.
Waandamanaji hata hivyo wameapa kuendelea kuandamana hadi Rais Yanukovych atakapojiuzulu.
Na BBCSwahili
Wakutana lakini hawasemezani

Wakutana lakini hawasemezani

Lakhdar Brahimi akiwaeleza waandishi wa habari kuwa wajumbe wa Syria watakutana chumba kimoja
Wajumbe wa pande mbili zinazopigana vita nchini Syria wanaohudhuria mkutano wa amani mjini Geneva walikutana kwa muda mfupi.

Walikaa chumba kimoja huku wamekabiliana, lakini hawakuzungumza moja-kwa-moja isipokuwa kwa kuptia mpatanishi wa Umoja Mataifa, Lakhdar Brahimi.
Kikao hicho cha kwanza kilidumu nusu saa tu, na mpatanishi pekee ndiye aliyezungumza. Mwandishi wa BBC mjini Geneva anasema utaratibu huo umewekwa ili kuepusha ugomvi kati ya wajumbe; na itifaki hiyo itafuatwa katika vikao vijavyo.
Wajumbe wakitarajiwa kukutana tena Jumamosi, na watalenga namna ya kufikisha misaada kwa wanyonge na kuwaachilia huru wafungwa wa kisiasa.
Upinzani unasema utaomba kuwa mapigano yasitishwe katika mji wa Homs.
Na BBCswahili
 Suala la mabadiliko ya tabia nchi lapewa kipaumbele Davos

Suala la mabadiliko ya tabia nchi lapewa kipaumbele Davos

Viongozi wanaokutana katika Kongamano la Kimataifa la Kiuchumi mjini Davos, Uswisi, wamelipa kipau mbele suala la kushinikiza kuimarishwa uchumi wa ulimwengu na kupunguza kiwango cha joto duniani kwa kuzingatia vyanzo safi vya nishati. 
Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, Christiana Figueres, amesema uchumi wa ulimwengu uko hatarini, kama hapatakuwepo na muafaka mjini Paris mnamo mwaka wa 2015 wa kupunguza kiwango cha gesi ya sumu kutoka kwenye makaa ya mawe na mafuta.
Mkutano huo ambao umeng'oa nanga hii leo, unahudhuriwa na zaidi ya viongozi 40 wa nchi na serikali pamoja na mawaziri wengi wa mambo ya kigeni kutoka kote ulimwenguni. 
Kwa mara ya kwanza katika mwongo mmoja, Rais wa Iran, Hassan Rouhani, atapewa fursa ya kulihutubia kongamano hilo hapo kesho. 
Rouhani anatarajiwa kuzungumza kuhusu mpango wa nchi yake wa nyuklia pamoja na nafasi za uwekezaji kwa makampuni ya kigeni.
EU yaionya serikali ya Ukraine dhidi ya ukandamizaji

EU yaionya serikali ya Ukraine dhidi ya ukandamizaji

Rais wa Halmashauri ya Ulaya Jose Manuel Barroso ametoa wito wa kusitishwa machafuko nchini Ukraine na akaionya serikali ya nchi hiyo kuwa Kamati Kuu ya Umoja wa Ulaya itatathmini "uwezekano wa kuchukuliwa hatua". 
Barroso amesema wameshtushwa na habari za karibuni kutoka Ukraine ambako waandamanaji wawili wameuawa mapema leo wakati polisi walipoivamia kambi moja ya maandamano na kuanza kupambana na waandamanaji wanaoipinga serikali. 
Rais Viktor Yanukovich leo anakutana na viongozi wakuu wa upinzani, ikiwa ni siku moja baada ya kufutilia mbali uwezekano wa kufanya mazungumzo ya aina hiyo. 
Wakati huo huo Waziri Mkuu wa Ukraine Mykola Azarov amewashutumu waandamanaji wanaoipinga serikali akiwaita kuwa ni "magaidi". 
Maelfu ya Waukraine wamefanya maandamano mjini Kiev tangu rais Yanukovich alipokataa kusaini mkataba wa ushirikiano wa kibiashara na Umoja wa Ulaya, na badala yake akaimarisha mahusiano na Urusi.
Umoja wa Ulaya kutuma kikosi CAR

Umoja wa Ulaya kutuma kikosi CAR

Umoja wa Ulaya umekubali kutuma wanajeshi 500 katika Jamhuri ya Afrika ya Kati katika juhudi za kusaidia kurejesha amani.
Uamuzi huo ulipitishwa baada ya wabunge katika jamhuri hiyo kumchagua meya wa mji mkuu, Bangui, Catherine Samba Pinza kuwa rais wa mpito wa nchi hiyo, akichukua nafasi iliyoachwa na Michel Djotodia, kamanda wa wanamgambo wa Seleka aliyejiuzulu mwezi huu.
Mgogoro ulianza katika Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya wanamgambo wa kiislamu kuchukua hatamu za uongozi wa nchi.
Ujumbe wa Umoja wa Ulaya utaungana na wanajeshi 1,600 wa Ufaransa na wengine wapatao 4000 kutoka mataifa ya kiafrika ambao tayari wamewasili nchini humo. 
Mkuu wa Sera wa Umoja wa Ulaya Catherine Ashton amesema wanajeshi wao watafanya kazi katika mji mkuu Bangui kwa muda wa hadi miezi sita, wakisaidia  kulinda usalama wa watu wa Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Kategori

Kategori