Elimtaa Tv: Kama unadeni katika sim kadi yako hauta hama Mtandao

WATANZANIA zaidi ya elfu 10 wametumia huduma ya kuhama mtandao mmoja kwenda mungine hudua mambayo imeziduliwa mwaka huu mwezi Machi huku kukudaiwa kuwa watu wengine zaidi ya 1000 wamekuwa wazizuiwa kuhama kutokana na matatizo mbalimbali yakiwemo madeni.

Huduma ya kuhana na mtandao pamoja na namba yako NMP unaruhusu mtumiaji wa simu kuhama namba yake kwenda mtandao mwingine ila kama anadeni hato ruhusiwa kuhama.

Waandishi wa habari wanapatiwa somo ili elimu hii kuwafikia wananachi wengine na huduma hiyo wakisema itawasaidia kuhamia mtandao wenye huduma wazipendazo.

Maofisa kutoka mamlaka ya mawasiliani hapa nchini TCRA wanasema kuwa mfumo huu utasaidia huduma kuwa bora kwa kuwa hakuna mtandao utakaokubari wateja kuhama.


Huduma ya kuhamia mtandao mwingine bila kubadili namba ya simu ya Kiganjani MNP inamaanisha kuwa mtumiaji wa simu anahama mtandao na huduma zake na kuhamia mtandao mwengine akiwa na namba yake ile ile na waliokuwa wakimpata kwa namba yake wataendelea kumpigia na haina haja ya kuwajulisha kama unahama.