TEMEKE IMEFANIKISHA KUINGIZA TIMU ROBO FAINALI NDONDO CUP 2017

Hatimaye wilaya ya Temeke imefanikiwa kuingiza timu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ndondo Cup 2017 baada ya Keko Furniture kuifunga Boom FC kwa changamoto ya penati katika hatua ya 16 bora.
Keko Furniture imekuwa timu pekee kutinga robo fainali ya Ndondo Cup msimu huu kufuatia timu nyingine za Temeke kuondoshwa.
Mechi kati ya Keko Furniture vs Boom imepigwa kwenye uwanja wa Kinesi mta wa Victor Wanyama. Keko walianza kupata goli la kuonoka dakika ya 35 kipindi cha kwanza likifungwa na Kashkashi Hashim.
Said Issa akaisawazishia Boom dakika ya 62 na mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 ndipo ikabidi mikwaju ya matata kuamua timu itakayosonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.
Katika changamoto ya penati, Keko walifanikiwa kufunga penati mbili wakati Boom wao walifanikiwa kufunga penati moja na kujikuta wakiyaaga mashindano ya Ndondo Cup 2017.

from Blogger http://ift.tt/2uUGltg
via IFTTT