WENGER AMGANDA KAMA RUBA ALEXIS SANCHEZ

Bado tetesi zinazidi kuongezeka kwamba Sanchez anaondoka Arsenal huku ikisemekana yuko njiani kuelekea nchini Ufaransa ambapo timu ya PSG iko tayari kuwalipa Gunners £70m ili kumnununa Sanchez.
Lakini kama unadhani kiasi hiko cha pesa ni kikubwa sana kiasi cha kumshawishi Wenger baasi utakuwa umekosea sana kwani Wenger hataki pesa hiyo na anachotaka yeye ni Sanchez tu.
Jana baada ya mchezo zidi ya Chelsea kocha huyo aliulizwa kuhusu habari za Sanchez kuzagaa kwamba anakwenda PSG lakini kocha huyo akasema hizo ni taarifa tu za vyombo vya habari.
Waandishi walimuuliza Wenger vipi kama PSG watato pesa ndefu zaidi ya Man City na ukizingatia kwamba PSG hawatokei Uingereza ambapo bado Wenger alisema uamuzi wake utabaki hivyo hivyo.
Arsenal wamerejea nchini Uingereza hapo jana na labda Wenger na Sanchez wataonana wiki ijayo kufanya mazungumzo, Wenger hataki kumuuza Sanchez kutokana na kiwango chake huku msimu uliopita akifunga mabao 30 na kutoa assist 19.

from Blogger http://ift.tt/2vMZ7zi
via IFTTT