Showing posts with label 2017 at 11:30AM. Show all posts
Showing posts with label 2017 at 11:30AM. Show all posts
TEMEKE IMEFANIKISHA KUINGIZA TIMU ROBO FAINALI NDONDO CUP 2017

TEMEKE IMEFANIKISHA KUINGIZA TIMU ROBO FAINALI NDONDO CUP 2017

Hatimaye wilaya ya Temeke imefanikiwa kuingiza timu katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Ndondo Cup 2017 baada ya Keko Furniture kuifunga Boom FC kwa changamoto ya penati katika hatua ya 16 bora.
Keko Furniture imekuwa timu pekee kutinga robo fainali ya Ndondo Cup msimu huu kufuatia timu nyingine za Temeke kuondoshwa.
Mechi kati ya Keko Furniture vs Boom imepigwa kwenye uwanja wa Kinesi mta wa Victor Wanyama. Keko walianza kupata goli la kuonoka dakika ya 35 kipindi cha kwanza likifungwa na Kashkashi Hashim.
Said Issa akaisawazishia Boom dakika ya 62 na mchezo kumalizika kwa sare ya 1-1 ndipo ikabidi mikwaju ya matata kuamua timu itakayosonga mbele kwenye hatua ya robo fainali.
Katika changamoto ya penati, Keko walifanikiwa kufunga penati mbili wakati Boom wao walifanikiwa kufunga penati moja na kujikuta wakiyaaga mashindano ya Ndondo Cup 2017.

from Blogger http://ift.tt/2uUGltg
via IFTTT


Video…Waziri wa Magufuli Atoa Povu Kuhusu Kuhusishwa na Video Inayomuonyesha Makonda Akingia Clouds Media Akiwa na Msururu wa Askari..!!

Waziri Mwijage akikanusha ujumbe wa Twitter ambao ulionyesha kuwa ulitoka kwenye akaunti yake kuhusu suala la Makonda kuonekana akiingia kwenye ofisi ya Clouds Media na askari.
Sasa ni nani aliyezusha hiyo kitu kuwa Mwijage ndo kaandika hivyo? Mwijage kasema yeye hana kabisa akaunti huko Twitter.

from Blogger http://ift.tt/2nUwDiS
via IFTTT


Ehe..Umesikia Alichosema Mwakyembe Juu ya Wizara Yake..?

Ehe..Umesikia Alichosema Mwakyembe Juu ya Wizara Yake..?

Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema tangu aingie katika wizara hiyo, wameboresha mazingira ya kisheria na ya mahakama.
Akizungumzia mjini Morogoro katika ziara ya siku mbili, pia ametoa wito kwa wananchi kuwaripoti mahakimu wanaokwenda kinyume kwenye kamati za maadili ambazo zimeundwa kila wilaya zikiwa chini ya wakuu wa wilaya ambao ni wenyeviti na makatibu tawala wa wilaya ni makatibu.
“Mkiwaona mahakimu ama kwa vitendo vyao, mwenendo, matamshi au wanakiuka kutenda haki, muwaripoti katika kamati hizi ambazo zina nguvu na zimeundwa maalumu kupunguza malalamiko ya wananchi. Uamuzi wa kamati hizi unakwenda hadi Tume ya Utumishi ya Mahakama,” amesema.
Akizungumzia biashara ya fedha, amewaonya wananchi kutojihusisha na kukopesha fedha bila kuwa na kibali cha Benki Kuu ya Tanzania (BoT), kwa kuwa ni kujihusisha na biashara haramu jambo ambalo halitavumiliwa.
Awali, Dk Mwakyembe amesema kuanzia mwezi Mei hakutakuwa na ndoa itakayofungwa nchini bila wahusika kuwa na vyeti vya kuzaliwa, lengo likiwa ni ili Taifa liweke vizuri kumbukumbu za raia wake.
Amewataka watu waliotajwa kisheria kuwa wanaweza kufungisha ndoa, wajiandae kutekeleza agizo hilo na kwamba uamuzi huo utakuwa ni wa lazima kwa kila mwananchi

from Blogger http://ift.tt/2mWqLbp
via IFTTT


Kategori

Kategori