CHELSEA WAWATAKA RADHI WACHINA BAADA YA KIUNGO WAO KUWAKASHIFU

=Chelsea wako nchini China kwa ajili ya mechi za kujiandaa na msimu mpya wa ligi lakini wakiwa nchini humo kiungo wao Kennedy amepata dhahma kubwa baada ya kuzomewa na raia wa nchi hiyo.
Kennedy ameingia katika matatizo hayo baada ya kusambaa kwa video ambayo ilimuonesha akiwadhihaki Wachina na nyingine inayoonesha kuwaita Wachina “wapumbavu” suala lililowaudhi sana raia hao.
Baada ya tukio hilo klabu ya Chelsea wametoa taarifa ya wazi kuomba msamaha kwa tukio alilofanya kiungo huyo na wakasisitiza kwamba hakuwa na nia ya kuwakosea heshima Wachina.
“Chelsea tunaomba radhi kwa video alizopost Kennedy jana jioni, hii ni tabia ambayo hatukuitarajia kwa mchezaji wetu lakini na yeye mwenyewe anajutia kwa tukio lililotokea tunaomba msamaha kwa hilo”
“Kila mtu katika klabu yetu ana heshima kwa taifa la China kwani wamekuwa wenyeji wema kwetu na wametuonesha upendo na uungwana wa hali ya juu, tunaomba msamaha” ilisema taarifa ya klabu ya Chelsea.
Hii leo Chelsea walikuwa na mechi zidi ya Arsenal ambapo wameibuka na ushindi wa mabao matatu kwa nunge mabao yakifungwa na Mitchy Batshuayi aliyefunga mbili na Willian akifunga lingine.

from Blogger http://ift.tt/2eFigQk
via IFTTT