Kondakta Afariki Dunia Na Wengine 21 Akiwemo Dereva Kujeruhiwa Katika Ajali Ya Basi Songea

Mtu mmoja amefariki dunia na wengine 21 kujeruhiwa kwa ajali ya basi katika maeneo ya Hangangadinda Songea baada ya dereva wa basi la
kampuni ya Superfeo Bw.Ally Ramadhan ally kuendesha gari mkono mmoja na mwingine kuutumia kufanya mawasiliano ya simu huku ajali hiyo
ikiwa imetokea siku moja baada ya gari la kampuni hiyo kupata ajali na kuua mtu mmoja kilomita 5 toka ilipotokea ajali ya kwanza.

 Aliyepoteza maisha katika ajali ya basi hilo aina ya Hiang lililokuwa likitokea mkoani Mbeya kuja Songea ni kondakta wa gari hilo Hassani
Ngonyani aliyechomoka kwenye mlango wa gari hilo baada ya kumshinda dereva na kuingia porini na kudondosha kifaa kimoja kimoja likigonga
miti porini huku majeruhi mmoja akilazwa wodi ya wagonjwa mahututi .
Meneja huduma wa kampuni ya Super Feo bw.Francis Sengo anasema wamesikitishwa na ajali hiyo kwa kuwa imetokea siku moja baada ya
kutokea ajali ya kwanza iliyoua dereva wao Ismail Nyami ambapo watoto wadogo wamenusurika kwenye ajali hiyo kwa miujiza ya mungu.

Mkuu wa wilaya ya Songea Bw.Pololeti Kamando Mgema aliyetembelea Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Ruvuma kuwaona majeruhi ameagiza
madereva kuanza kupimwa kilevi na kupendekeza madereva wanaosababisha ajali kunyang’anywa leseni ambapo dereva aliyesababisha ajali hiyo
Bw.Ally Ramadhani anatibiwa chini ya ulinzi wa polisi ili akimaliza matibabu aweze kufikishwa mahakamani.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sPM9jK
via IFTTT