Wahamiaji haramu 10 mbaroni,magunia 120 ya mkaa yakamatwa Sengerema

Operesheni ya kuwasaka watu wanaoharibu Hifadhi ya misitu ya Taifa,ikiwemo kujihusisha na kilimo cha zao
haramu la bangi ndani ya misitu hiyo inayomilikiwa na wakala wa huduma za misitu tanzania ( TSF ) katika
kisiwa cha Meisome wilayani Sengerema mkoani Mwanza,imewezesha kukamata wahamiaji haramu
10,magunia 120 ya mkaa pamoja na kuharibu matanuru matano ya mkaa. 

Operesheni hiyo iliyoendeshwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Sengerema kwa kushirikiana na
ofisi ya wakala wa huduma za misitu wilayani humo,inalenga kunusuru uharibifu wa msitu wa hifadhi wa
Maisome,kubaini na kuteketeza mashamba ya bangi,kilimo,uvunaji haramu wa mazao ya misitu,uvuvi haramu
pamoja na kuwakamata wahamiaji haramu.

Mkuu wa wilaya ya Sengerema Emmanuel Kipole,akizungumza na wananchi wa kijiji cha Kisaba katika
mkutano wa hadhara muda mfupi baada ya mkazi wa kijiji hicho Isack Paschal kukamatwa na magunia 90 ya
mkaa nyumbani kwake, 
huku kikosi kazi hicho kikifanikiwa pia kuteketeza robo heka ya shamba la bangi
lililokuwa linamilikiwa na raia mmoja kutoka nchi jirani ya Burundi,amewataka wananchi kulinda msitu huo na
kupiga vita uvuvi haramu ndani ya Ziwa Victoria.
Operesheni hiyo ambayo ni endelevu halikadhalika imewanasa wavunaji haramu wa mazao ya misitu wapatao
sita, 
msumeno mmoja,nyavu haramu 50 aina ya timba,kokoro moja,tani moja ya samaki wachanga aina ya
sangara ambapo taratibu za kisheria za kuwafikisha mahakamni zimeanza kufanyika. 
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2sa8giX
via IFTTT