TAARIFA KUHUSU RUFAA ZA WATUMISHI WALIOKUTWA NA VYETI FEKI

Serikali imesema kuwa watumishi wa serikali ambao wamekutwa na vyeti feki na kukata rufaa wakielezea kuwa vyeti vyao ni halali, itajulikana mwezi huu mwishoni ambapo uamuzi kuhusu rufaa zao utatolewa.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dk Laurian Ndumbaro alipokuwa akiongea na watumishi wa halmashauri sita za Mkoa wa Simiyu wakati wa ziara yake ya siku moja mkoani humo.
Kiongozi huyo alisema mchakato wa kuvihakiki unakaribia kumalizika na karibuni uamuzi kuhusu wao utatolewa.
“Tunatarajia hadi kufika Juni 30 mwaka huu, wale wote ambao walikata rufaa baada ya kubainika kuwa na vyeti vya kughushi tutatoa majibu ya rufaa zao, ambazo tulikuwa tukiendelea kuzipitia kwa makini.”
Watumishi hao 9,932 waliokuwa katika orodha aliyokabidhiwa Rais Magufuli walitakiwa kuondoka katika utumishi wa umma baada ya kubainika kuwa na vyeti vya kughushi.
Wale ambao waliona kuwa wameonewa walipewa nafasi ya kukata rufaa ambapo ndio maamuzi ya rufaa zao yatatolewa mwishoni mwa mwezi huu.
ASANTE KWA KUTEMBELEA MTANDAO WETU!!

from Blogger http://ift.tt/2t8Nepn
via IFTTT