Warajisi walalamikiwa kuto kuwa makini chanzo vyama vya ushirika kufa


WARAJISI wa Vyama vya Ushirika wa wilaya nchini wamedaiwa kuwa ni wazembe na chanzo cha vyama hivyo kufirisika kwa kuto kuwa wasimamizi wazuri na kushituka vyama hivyo mimesha baki vitupu na kukaribia kufa.

Hayo yanaibuliwa na wanasakosi wa chama cha ushirika cha wafanyabiashara   Njombe ambacho kimefirisika na fedha za wanachama huku kikubakia na madeni ya zaidi ya milioni 800 za wanachama na fedha kutoka taasisi za kifedha.

Katika mkutano wa Dharula uliowakutanisha wananchama na warajisi wa Kitaifa na mkoa wa Njombe wa kusoma taarifa ya Mapto na Matumizi ya Chama Hicho zinaibuka lawama kwa warajisi


Walioweka fedha kwa malengo ya kusomesha na kuibua miradi yao wanasikitika kushindwa kufikia matarajio ya kuweka fedha katika chama hicho.

Bodi ya chama hicho inadaiwa kukopesha fedha bila kufuta vigezo vya kutoa mkopo na kusababisha Saccos hiyo kufirisika ambapo mikopo hiyo ilitolewa kinyume cha sheria.


Kutokana na kuibuka kwa hayo Bodi ya chama hicho inavunjwa na kaimu Mrajisi Msaidizi wa udhibiti wa vyama vya ushirika wa kifedha Tanzania na bodi mpya inaundwa ili kufuatilia fedha hizo.