SERIKALI KUJENGA MABWENI CHUO CHA VETA MAKETE

 NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA Eng STELLA MANYANYA AKIPITIA VIFAA VYA KUFUNDISHIA VYA CHUO CHA VETA MAKETE MKOANI NJOMBE


MKUU WA CHUO CHA VETA MAKETE AKIZUNGUMZA NA WANAFUNZI BAADA YA KUPATA UGENI WA NAIBU WAZIRI WA ELIMU SAYANSI NA TEKNOLOJIA, Eng STELA MANYANYA.

SERIKALI imesema itajenga mabweni mawili katika chuo cha Veta wilaya ya Makete mkoani Njombe ujenzi huo unasaidia wanafunzi kudahiliwa kwa mahitaji cha chuo tofauti na sasa ambapo wanafunzi ni wachache ukilinganisha na uwezo wa chuo hicho.
Kauli hiyo ujenzi inatolewa na  Naibu waziri wa Elimu Sayansi na Teknologia, Eng. Stella Manyanya wakati akiwa katika ziara yake ya siku moja Chuoni hapo ambapo wanafunzi wake asilimia kubwa wanaishi nyumba za kupanga umbali wa zaidi ya kilomita moja.

Eng. Manyanya anasema kuwa katika bajeti ya serikali ya mwaka huu imetenga fedha kwaajili ya kujenga mabweni mawili katika shule hiyo.

Alisema kuwa lengo la ujenzi wa mabweni hayo ni kuhakikisha kuwa wanafunzi wengi wanapata nafasi za kusoma na kuwa sasa wanafunzi sio wengi ni kutokana na kuto kuwapo kwa mabweni shuleni hapo.

Wanafunzi nao wanakili kuto kuwepo kwa mabweni kuwa kunawaathili kimasomo na kupoteza muda wao kuinga darasani huku uongozi ukitaja hatua ulizofikiwa. 

Wanafunzi hao wengi wao ni kutoka nje ya mjini Makete na wengine ni kutoka nje ya mkoa wa Njombe ambao wote wamepanga katika wilayani Makete.

Mkuu wa schuo hiyo Ramadhani Sebo anasema kuwa chuo hiso sasa kipo katika hatua ya kutathiminiwa na wakandarasi juu ya gharama, na ujenzi utaanza baada ya wakadarasi kufanya tathimini zao.


Naye mbunge wa jimbo hilo Prof. Norman Sigala, anaye daiwa kuomba sana kujengwa mabweni anatoa shukrani zake kwa serikali na kuwa watoto wengi wamekuwa wakipata shida kwa kutoka mbali na shule wanapo kwenda shule.