Showing posts with label Mikoani. Show all posts
Showing posts with label Mikoani. Show all posts
Mfuga Joka afa baada ya joka lake kuuwawa
Mkazi wa Mtaa wa Mateka, Manispaa ya Songea, Denis Komba (26) afariki dunia baada ya nyoka wake aliyekuwa amembeba kwenye mfuko wa jaketi kuuawa na wananchi.

Komba alifariki dunia katika hospitali ya Rufaa Songea mkoa wa Ruvuma (Homso) ambako alilazwa baada ya watu wenye hasira kumuua kwa mawe na fimbo nyoka wake huyo.
Mashuhuda wanaeleza kuwa kabla ya wananchi kumuua nyoka huyo, Komba aliwasihi wasifanye hivyo kwa kuwa wakimuua na yeye angekufa, lakini ombi lake hilo halikusikilizwa.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, siku ya tukio Komba alikodi pikipiki ya Kassian Haule (24) ambaye ni mkazi wa Mpitimbi, yenye namba za usajili MC 724 AKB ili apelekwe nyumbani kwake mtaa wa Mateka.
Akisimulia tukio hilo, alisema alipofika katika eneo la Benki ya Posta ya zamani barabara kuu ya Sokoine, dereva wa pikipiki alihisi kuna kitu kinamtekenya na kumgonga gonga kwa nyuma, ndipo alipogeuka nyuma na kumwona abiria wake amebeba nyoka mkubwa huku amesimamisha kichwa.
Haule alisema, baada ya kumuona nyoka huyo aliruka kutoka kwenye pikipiki na kuanguka pembeni mwa barabara na abiria wake alimwachia yule nyoka ambaye alikimbilia kwenye kalavati la maji.
Aliongeza kuwa ndipo alipopiga kelele za kuomba msaada na kundi la vijana waendesha pikipiki wenzake walifika eneo hilo la tukio kwa lengo la kumsaidia mwenzao juu ya maswahiba yaliyompata hadi kumfanya apige kelele.
Alisema kabla ya vijana hao hawajafanya jambo lolote, Komba aliwaomba vijana hao na watu wengine waliofika katika eneo hilo wasimpige nyoka wake kwani iwapo watampiga na kufa yeye pia atapoteza maisha. Kutokana na maneno hayo, Haule alimtoa nyoka huyo ndani ya kalavati na kwa kushirikiana na vijana wenzake walianza kumpiga nyoka huyo hadi kufa.
Alisema wakati wanampiga nyoka huyo, Komba ambaye ndiye mmiliki wa nyoka huyo naye alianza kulegea kisha akaanguka chini huku akitokwa na mapovu mdomoni na puani.
Habari zinasema kuwa,baada ya Komba kuanguka alikimbizwa hospitali kwa ajili ya kupatiwa matibabu; hata hivyo juhudi za madaktari na wauguzi wa hospitali za kuokoa maisha yake zilishindikana kwani Komba alifariki.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Ruvuma, Zuberi Mwombeji, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa mwili wa marehemu haukuwa na jeraha lolote na umehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhi maiti katika hospitali ya rufaa Songea.
Alisema nyoka aliyeuawa na wananchi amechukuliwa na idara ya maliasili na uchunguzi zaidi ya tukio hilo unaendelea ili kubaini kiini cha tukio hilo la kuuawa kwa nyoka na kisha mmiliki wake naye kufa. Kamanda Mwombeji alisema, kwa upande wa dereva wa pikipiki yeye anaendelea vizuri na anapatiwa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Ruvuma.
Aidha Kamanda Mwombeji, ametoa rai kwa wananchi kuacha mara moja kumiliki nyara za serikali zinazoweza kuwaletea madhara kama vile majeraha au vifo.
WANANCHI WA LUGENGE WATEMBELEA CHANZO CHA MAJI
SIKU chache baada ya wananchi kuomba mradi wa maji ukamilike haraka wamemuomba Rais Kutimiza ahadi yake aliyo itoa akiwa katika viwanja vya Sabasaba Mkoani Njombe na kuamua kufika mpaka katika chanzo cha maji ili kuona maendeleo ya mradi huo.
Wananchi baada ya kufika katika chanzo cha maji wanabaini kuwa mradi huo bado kukamilika kwa kuwa mabomba kutoka katika chanzo hicho bado huku chanzo kingine kikiwa na mashaka kutokana na kilipo na maji yanayopatikana katika chanzo hicho yakiwa ni machache wanawasiwasi wa kuwapo kwa ubadhilifu.
TAZAMA VIDEO HAPA CHINI
Wakiwa katika chanzo cha pili cha maji wananchi wanashangaa kuona chanzo kilomo na mabomba yanao elekea kuona kuwa kuna mlima ambako maji yanatakiwa kupita na kuwa na wasiwasi wa maji kutoka katika chanzo hicho cha pili na kutokana na maji yanayo zalishwa katika chanzo hicho.
Wakiwa katika chanzo cha pili cha maji wananchi wanashangaa kuona chanzo kilomo na mabomba yanao elekea kuona kuwa kuna mlima ambako maji yanatakiwa kupita na kuwa na wasiwasi wa maji kutoka katika chanzo hicho cha pili na kutokana na maji yanayo zalishwa katika chanzo hicho.
Kinacho wasukuma wananchi hao kufika mpaka katika chanzo cha maji ni kutokana majibu waliyo pata kutoka kwa mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe ambaye aliwaambia bado kilometa saba maeneo ya kutoka kijijini hapo ambapo kuna mabomba ya maji.
Mmoja wa wazee walio fika katika chanzo hicho kilichopo kilimota zaidi ya 20 kutoka kijijini pao Festus Mdoche, anasema kuwa kwakweli kazi bado ni kubwa kwa kuwa katika chanzo mabomba bado hayajafukiwa na kijijini bado kusemekana bado kilometa saba anawasiwasi.
Alisema kuwa pamoja na kuwa kazi bado sana lakini mabomba yal;iyoko maeneo ya chanzo yamepigwa na jua kiasi kwamba yanaweza kuvunjika haya yakigongwa na jiwe kwa kuwa yamekaa muda mrefu juani.
“Kwa kweli kusema bado kilometa saba mimi siamini kwa kuwa huku kwenye chanzo mabomba hayajafukiwa na kwa pale kijijini bado napo hapajafukiwa tunawasiwasi kuwa mradi huu utakamilika mapema,” alisema Mdoche.
Aidha wananchi hawa wanasema kuwa maji wanayotumia kwa sasa ni maji hatari kwa afya yao kwa kuwa wanashiriki pamoja na Mifugo yao.
Akiwa kijijini hapo Matha Malechela, mkazi wa Lugenge anasema kuwa sasa wapo hatarini kupatwa na magonjwa kwa kuwa pamoja na kufuata maji umbari mrefu pia wamekuwa wakitumia maji pamoja na mifugo yao ambapo mifugo hunywa kwa juu huku wao wakichoto kwa chini.
Wanaomba rais Kukumbuka ahadi aliyo waahidi katika mkutano wa hadhara wakati za kampeni oktoba 2015 ambapo rais alimwita mbunge wa jimbo la Njombe na kumuuliza kelo na mbunge alisema kuwa ni maji ya Lugenge ambayo mpaka sasa bado maji hayo.
Mtoto Benito Benadito, anasema kuwa wamekuwa wakitumia muda mwingi kutafuta maji wakitoka na asubuhi kabla ya kwenda shule kwa ajili ya kufanya usafi wao na madarasa wakiwa shuleni hivyo anamuomba rais kuwasaidia kusukuma mradi huo wa maji ili yawafikie.
Hata hivyo Mwenye halmashauri anasema kuwa tatizo ni mkandarasi kutokuwa na fedha na serikali inalipa baada ya kukamilisha kazi.
Anasema wananchi wavumilie kwa kuwa mradi wao huo ni moja ya miradi ya vijiji kumi ambayo inatakiwa kukamilika lakini mradi wao umefikia katika hatua nzuru na kunavijiji ambavyo miradi bado haijaanza.
Subscribe to:
Posts (Atom)
