Vituko sokoni panya bira woga anatalii kwenye matunda
Onesmo Katoro mfanyabiashara soko kuu Njombe
Isakwisa Edward makamu mwenyekiti soko kuu Njombe akiwa katika eneo lake la biashara
GARI YA TAKA IKIWA MTAANI KUKUSANYA TAKA KWA WANANCHI
Mathias Gambishi, Afisa afya mkoa Njombe
MIEZI michache baada ya kuanzishwa kwa utaratibu wa kupitisha
gari mitaani na sokoni kukusanya taka zilizo hifadhiwa na jamii badala ya
kuwekwa kwenye vizimba wafanyabiashara katika soko kuu la Njombe wanawasiwasi
wa kupata magonjwa ya mlipoko mvua zikianza.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti tuu ja mpango huo wanasema
kuwa mfumo huo ni mzuri kwa sasa kwa kuwa amvua bado hazijaanza kunyesha na
watu wanahifadhi taka wao wenyewe mpaka gari itakapofika.
Onesmo Katolo anasema kuwa mfumo huo ni mziri lakini shida ni
kutaa na taka mwa muda wa zaidi ya siku nne hadi tano wakati gari haijaja
katika maeneo yao ambalo hupita maramoja kwa wiki ambapo likijitahidi sana huja
mara mbili.
Alisema kuwa kukaa sana na taka ni bora na mfumo ule wa kwa
nza kwa kuwa sasa nzi na wadudu wengine wanazaliwa karibu na mazingira yao ya
bisahara na kuwa mvua zikianza halmshauri iongeze siku za kuja kuchukua taka
katika maeneo yao kwa kuwa taka hizo watashindwa kuzitunza.
Kaimu mwenyekiti wa soko kuu la Njombe Isakwisa Edward
alisema kuwa mfumo huo unasaidia kwa kuwa sasa taka katika kizimba chao ambzo
zilikuwa ni kelo sasa hakuna kazi inabaki kwa halmashauri kuboresha mfumo huo
kwa kuongeza gari ya taka ili siku za kupita sokoni hapo zikaongezeka.
Alisema kuwa kwa mfumo huo kuanzia kipindi cha mvua
kunahatari ya kupatikana kwa hatari ya kupatikana kwa magonjwa kwa kuwa
magonjwa yatazalishwa katika vibanda vya watu hivyo mfumo huu kwa kipindi cha
mvua kuongezwe gari za kupita sokoni.
Utaratibu huo unaingia katika mwezi wa tatu ukionyesha
mafanikio ya kuto kuwapo kwa mrundikano wa taka katika vizimba ambazo sasa taka
hazitupwi huko.
Afisa afya mkoa wa Njombe, Mathias Gambishi anasema kuwa
utaratibu huo umeanzishwa kwa majaribio baada ya halmashauri kuona inazidiwa na
utoaji wa taka katika vizimba.
“Utaratubu huu unafanyika kwanza kwa halmashauri ya mji
Njombe na utahamia katika halmashauri zinging baada ya kuona mafanikio yake
katika halmashauri hii ya Mji Njombe,” alisema Gambishi.
Aidha Gambishi aliongeza kuwa utaratibu za vizimba ulikuwa ni
kelo kwa wanchi kwa kuwa taka zilikuwa zinakaa kwa muda mrefu na sasa
zinaondolewa na kuwasaidia wananchi wa mitaa iliyo kuwa katibu na vizimba hivyo
kuto kuwa na adha hiyo ya harufu chafu.
Alisema kuwa pia katika vizimba hivyo vilikuwa vikibomoka
taka zinapo ondolewa na katapila na kuwa ni mazalia ya Nzi na panya pamoja na
wadudu wengine wabaya.
Hata hivyo baadhi ya wakazi wa mitaa ya mjini Njombe wanasema
kuwa utaratibu huo ni nafuu kwao kwa kuwa unawaepusha na tatizo la mrundikano
wa taka vizimbani.
Wamesema utaratibu huo unawaondolea uvifu wa kutupa taka
vizimbani kwa kuwa gari inawafuata majumbani kwao moja kwa moja na gara kutupa
kule zinako hitajika kutupwa na mitaa kuwa misafi.