WADAU WAOMBWA KUJITOKEZA KUKARABATI MIUNDOMBINU YA AFYA

MKUU wa wilaya ya Njombe Ruth Msafiri anaomba jamii kujitokeza kuisaidia serikali pale  inapo ona inaweza kusaidia hasa katika miundombinu mbalimbali ya kijamii.

Anasema kuwa serikali haitamzuia mtu yeyote anayejitokeza kufanya ukarabari wa mali za umma ila tu atakaye bainika kuharibu itakula naye sahani moja kwa kuchukua atua za kisheria dhidi yake.

Msafiri anatoa kauli hiyo wakati akifungua kazi ya kuanza kukarabati jingo la gredi ya kwanza katika hospitali ya Kibena ambayo ukarabati unafanywa na watu watatu waliolidhishwa na huduma aliyopatiwa ndugu yao.

Alisema kuwa ni watu wachache wanao kumbuka fadhira za kutendewa mema na wale walio fanyiwa huduma vizuri ndia wanao toa shukrani kuliko wale watakaopata huduma kwa kutoa rushwa.

Alisema kuwa haita kuwa rahisi kwa mtu ambaye amepata huduma kwa kunyanyashwa akarudi kushururu hivyo hospitali ione imetoa huduma vizuri kwa watu hao na kuendereha hivyo na kwa watu wengine.

Ndugu hao wanasema hii ni shukrani na vyumba vitatu vitawekwa tailizi, na kupakwa rangi paa la jengo na ukarabati mwingine katika maeneo mbalimbali ya vyumba vya hospitali hiyo ikiwa ni pamoja na kupaka rangi dali za vyumba hivyo.

Akisoma taarifa ya vitu watakavyo fanya kwa niaba ya wenzake wawili Elly Ngole alisema kuwa watakarabati vyumba vitatu kwa kuweka Tailizi, kupaka rangi, kupaka rangi bati, na kukarabati baadhi ya vyoo.

Hata hivyo Ray Mbogailonguwe, alimtoa wasiwasi kuwa baada ya kuweka Tailizi milango yote itakuwa kama kawaida kwa kuwa sakafu itachimbuliwa kidogo na kumuomba mkurugenzi kuwasogezea mchanga kwa kuwa halmashauri ina Gari.
  
Watu hao wanao jitorea kukarabati waliuguza shangazi yao hapo na kupata rufaa ya kwenda kutibiwa hospitali ya taifa ya Muhimbili, ambao ni Ray Mbigailonguwe, Elly Ngole na Njowoka huku Ukarabati huo unaanza mara moja baada ya kufunguliwa na mkuu wa wilaya huyo ambapo uboreshaji huo utahitajika wagonjwa kuto tumia vyumba vinavyo karabatikwa mpaka ukarabati unapo kamilika.

Kwa upande wa hospitali hiyo iliyo jengwa kabla ya uhuru inaonyesha kuchoka na kama imesahauriwa, waungwana hao wanashukuriwa na uongozi  wa hospitali, halmashauri na kamati ya afya halmashauri ya mji wa Njombe.

Kwa niaba ya mkurugenzi Gwalbert Mbujiro anasema kuwa anashukuru kwa kuungwa mkoni kwa kuwa wao sasa wanaendelea na ukarabati wa maabara na kuwa wanahitaji sana kufanya ukarabati hospitali nzima lakini wanakwama kutokana na kuto kuwapo kwa fedha za kutosha.


Hata hivyo kwa niaba ya uongozi wa Hospitali Morice Mgaya, anasema wanaona umuhimu wa ukarabati huo kwa kuwa wagonjwa wengine walikuwa hawalazwi katika chumba kimoja kwa kuwa kulikuwa kimeharibika kabisa na sasa wanaona matunda ya kutoa huduma bora kwa kuwa wamekuwa wakipokewa lawama pekee na sio shukrani.