Meya wa jiji la Dar akamata Kiwanda kilichokwepa kulipa Mapato kwa Miaka 6

 Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita akisikiliza jambo kwa Meneja wa kiwanda hicho Tito Kasele mara baada ya kumaliza kukagua mitambo ya uzalishaji wa pombe aina ya Chibuku Jana ,ubungo jijini hapa.
 Meya wa Jiji la Dar es Salaam katikati akipata maelekezo kutoka kwa meneja wa kiwanda hicho Tito Kasele kushoto aliyeshika chumba ,wakati wa ziara ya kukagua mitambo inayozalisha pombe aina ya Chibuku. Kulia ni mbunge wa jimbo la Temeke Abdalha Mtolea akiwa na wajumbe wengine wa msafara huo.
Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita wa mwisho kushoto akipata maelekezo Juu ya mtambo unaozalisha pombe ya chibuku kutoka kwa meneja wa kiwanda hicho Tito Kasele aliyevaa Shati jeupe.

NA MWANDISHI WETU Dar
MEYA wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita amewaweka kiporo uongozi wa kiwanda cha Dar es Salaam Breweries Limited maarufu kama chibuku kilichopo ubungo jijin Dar es Salaam kutokana na kutopeleka mapato ya jiji kwa kipindi cha miaka sita

Hatua hiyo ilitokea jijini hapa jana , baada ya Meya Isaya kufanya ziara kwenye kiwanda hicho ikiwa ni mara ya kwanza tangu kuchaguliwa kwake yenye lengo la kuangalia mali za jiji na hivyo kukutana na changamoto mbalimbali.

Moja ya changamoto iliyofanya kuchukua hatua hiyo ni baada ya Meneja wa Kiwanda hicho Tito Kasele kutoa taarifa ambayo ilikuwa ikieleza kwamba tangu mwaka 2013 hakuna faida ambayo imepatikana na kuwapatia jiji.

Meneja huyo alisema kwamba katika kipindi hicho pesa ambayo ilikuwa ikipatikana ilikuwa ikitumika kununulia mitambo kwa ajili ya kuongeza ufanisi wa uzalishaji ,sambamba na uwekezaji jambo ambalo limefanya kwa kiasi kikubwa jiji kukosa mapato.

Mbunge wa jimbo la Temeke alihoji uongozi wa kiwanda hicho cha Chibuku kwamba ni kwa kiasi gani ambacho wanapata faida sambamba na jiji kunufaika na kiwanda hicho kutokana na umiliki wa hisa za asilimia 40 ndani ya kiwanda hicho , jambo ambalo halikupatiwa majibu na hivyo kuzuka kwa mzozo.

Kutokana na hali hiyo , Meya Isaya alisema kiwanda hicho kimekuwa kikilinyima jiji faida na hivyo kupata asara na hivyo kuwataka wajitathimini namna  ambavyo wanaendesha kiwanda hicho kabla maamuzi magumu hayaja fanyika.

" Hapa sikuja kupata siasa ambazo mtanipa hivi sasa, nimekuja kujua kwanini mnatunyima faida, tunataka kujua tunapata faida kiasi gani, matokeo yake ni hasara tu, hamuwezi kunidanganya kama mtoto mdogo wakati na jua kila kitu ambacho kinaendelea"

Hapa nikiangalia mhasibu hayupo ambaye alitakiwa kutoa taarifa ya fedha, mkurugenzi pia amenikimbia , naondoka lakini nitajua kitu gani cha kufanya, siwezi kuzungumza leo cha msingi mwambie Mkurugenzi anitafute mwenyewe , lakini pia mjitathimini upya nataka mapato nasio siasa" alisema Meya Isaya.

Hata hivyo haikufahamika mara moja kwamba nikiasi gani ambacho jiji imepata hasara kutokana na mfumo wa gawio ambalo wanapata kwa kila mwaka.

Awali Meya Isaya alitembelea eneo la Mbezi Luisi ambako inatarajiwa kujengwa kwa stendi kubwa ya mabasi na hivyo kutokana na hali ya eneo lilivyo alimshauri  Mkurugenzi kukaa na kamati yake kuona namna ambavyo wanaweza kuwalipa fidia wananchi ambao watatakiwa kuondoka ilimkupisha ujenzi