ZAIDI ya bilioni 300 hupotea kila mwaka kutokana magonywa yatokanayo na uchafu yakiwemo ya Kuhara na kisababisha watu vifo vya wato 30,000 hapa nchini, wakati dawa yake ni usafi wa mtu momoja moja na taasisi mbalimbalimbali za uma na binafsi.
Takwimu hizo zimetolewa na Katibu tawala mkoa wa Njombe Jackson Saitabahu, ambaye alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya siku ya usafi wa mazingira ambayo yamefanyika mkoani humo kitaifa na kuhudhuliwa na wizara ya Afya na elimu, pamoja na wadau mbalimbali.
Akizungumza na hadhara ya wakazi wa Njombe Saitabahu alisema kuwa watanzania wengi ambao ni nguvu kazi ya taifa kutokan ana magonjwa hayo ya kuhara ambayo kwa kufanya usafi sahihi wa mikoni hayawezi kuipata jamii ya watanzania.
Aliongeza kuwa hapa nchini ni asilimia 34 tu ya yaka ambazo zina vyoo bora na ndio maana magonjwa ya kuhara hayaishi hapa nchini, katika mikoa ambayo ugonjwa kipindupindu upo kuna wagonjwa, 8860 na watu 128 wamefariki dunia.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kinga Tanzania kutoka wizara ya afya, kwa niaba ya katibu mkuu wizara ya afya, Dr. Neema Lusibamayila alisema kuwa maazimisho hayo yamekuwa na wadau mbalimbali wa kutoa elimu na kufanya mashindano ya zahanati, masoko, bar, shule na sehemu zingine za kutolea huduma za afya.
Aliongeza katika mashindano yayo kuna maeneo yalipitiwa kufanyiwa tathinini ya usafi wa mazingira katika maeneo husika, na kutoa wito kwa jamii kutumia vyoo vizuri, na huhakikisha kuwa usafi wa mazingira inazingatiwa ili kuepuka na magonjwa yatokanayo na uchafu.