Muamivu ya hedhi huwaathiri wanawake wengi wakiwa kazini



Wanawake wengi huugua kimya kimyaImage copyrightSCIENCE PHOTO LIBRARY
Image captionWanawake wengi huugua kimya kimya

Wanawake wengi wamekabiliwa na maumivu wakati wa hedhi, hali inayoathiri uwezo wao kufanya kazi , utafiti unasema.
Utafiti huo wa YouGov uliohusisha wanawake 1,000 katika kipindi cha BBC, umegundua kuwa 52% waliuguwa, lakini 27% waliwaarifu waajiri wao kwamba ni mamumivu yanayotoka na hedhi.
52% pekee, karibu thuluthi yao waliomba kwenda nyumbani japo kwa siku kutokana na maumivu ya hedhi.
Na daktari mmoja amependekeza waajiri sasa waanze kutoa ''siku ya mapumziko ya hedhi'' kwa wanawake.
Wanawake 9 kati ya 10 wameeleza kuwahi kuugua maumivu ya hedhi kwa wakati mmoja.

kalenda ya mweziImage copyrightISTOCK

'Kuungulika kimya kimya'

Daktari wa magonjwa ya wanawake kutoka London Gedis Grudzinskas, anasema wanawake wanapaswa kuwa na uwazi zaidi kuhusu tatizo hili na waajiri wawe ni wenye kuwaelewa.
Ameongeza: "kupata hedhi ni jambo la kawaida, lakini baadhi ya wanawake huteseka sana kimya.
"sidhani wanawake wanapswa kuona haya kuhusu tatizo hili na kampuni zinapaswa kuwaelewa kwa naman wanavyotaabika kwa uchungu wanao uhisi."
Dr Grudzinskas anasema njia moja ni kutoa likizo au amapumziko ya hedhi kwa wafanyakazi wote wanawake kama ilivyo sasa kwa nchi kama Japan.
"Mapumziko hayo yatafanya kila mtu afanye kazi vizuri ambalo ni jambo lenye manufaa," amesema.
"Hakuna uelewa wa kutosha kuhusu maumivu au uchungu huo na kuwa huenda maumivu hayo wakatimwingine yanadhihirisha ugonjwa mkubwa zaidi ''.
"Watu husahau kuwa wanawake ni nusu ya nguvu kazi, iwapo watahisi wanaungwa mkono , itakuwa ni furaha na ufanisi wa kila mtu."