SERIKALI inaendelea
kupambana na magonjwa ya kuhara na Nimonia kwa watoto wadogo chini ya umri wa
miaka mitano kwa kutumia dawa zilizoboreshwa N a kufungashwa pamoja zinazoitwa
ZIORA zenye zink , ORS na amoxiline kwa ufadhili wa shirika linalo hudumia watoto Duniani Unicef.
Tafiti zinaonyesha
kuwa idadi Kubwa ya watoto chini ya miaka mitano wanakufa kutokana na
magonjwa haya ya Vichomi na kuhara ambayo kutokana na walezi kuchelewa
kuwafikisha sehemu za tiba na kuifanya wizara ya afya kuinuka maofisini na kuelekea
mikoani kufanya utafiti tangu mwaka 2013.
Baada ya uzinduzi wa Matumizi
ya dawa mpya ya Ziora katika kuendeleza mapambano dhidi ya magojwa hayo
ya kuhara na vichomi kwa watoto chini ya miaka mitano kitaifa jijini Dar es salaam
uliojumhisha waganga wakuu nchini watalam wa afya.
Wataalamu juzi
wataalamu wamefika mkoani Njombe na kutoa mafunzo ya uhamasishaji kwa watoa
huduma za afya ngazi ya mkoa na wilaya na kujumuisha viongozi wa serikali
wakiwemo wakuu wa wilaya na wakurugenzi.
Docta Rukia Ally (Pichani) ni mtaalamu
wa afya kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii alieleza lengo la mafunzo hayo
na kwamba yatakuwa endelevu katika mikoa mingine Hapa nchini ndani ya
miaka miwili ili kudhibidi vifo vya watoto.
“Walsha hii inalenga
kutoa hamasa ya kuhakikisha watoa hudyuma za afya wanatoa huduma sahihi za afya
kwa watoto na kuhakikisha vifo vitokanavyo na magonjwa haya vina koma,” alisema
Dr. Ally
Washiriki wa mafunzo
ya mapambano ya magojwa hayo wakiwemo wakuu wa wilaya, wakurugenzi na
wataalamu wa afya kutoka wilaya za Njombe na Makete, mkoani Njombe wametoa ushauri
kwa wizara kupeleka dawa mapema katika Hospitali, Vituo vya afya na Zahanati
pamoja na kubainisha gharama za mauzo ili ziwafikie walengwa mapema na kubaisha
changamoto katika utoaji wa huduma za afya maeneo yao ya kazi kama anvyoeleza
mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya makete Fransis Maumbo
Naye Katibu tawala
mkoa wa Njombe Jackison Saitabau, wakati wakifungua na kufunga mafunzo hayo
yaliyodumu kwa siku moja pamoja na kuwapongeza Unicef na kwa ufadhili
mkubwa wanaotoa kwenye sekta ya afya amewataka washiriki kutekeleza kwa vitendo
elimu walioipata pamoja na kifikisha kwa watumishi wengine wa afya na wazazi