DKT KIGWANGALLA ATOA USHAURI WAKE JUU YA UDHIBITI WA MADAWA SERIKALINI


Dkt Hamisi Kigwangalla Mbunge Mteule Nzega Vijijini CCM.


MBUNGE mteule jimbo la Nzega vijijini  Dkt Hamisi Kigwangalla  (CCM) ametoa ushauri kwa wizara husika juu ya udhibiti wa kuvuja kwa madawa serikalini na kwenda kwenye maduka binafsi.

Kupitia ukarasa wake facebook Kigwangalla amesema #‎Sasa Kazi Tu Changamoto ya Udhibiti wa Kuvuja Madawa Kutoka Mfumo wa Serikali Kwenda Kwenye Maduka ya Watu Binafsi ni Katika Mambo ambayo mgombea Urais wa CCM, Ndg. John Pombe Magufuli alionesha kuwa yanamkera sana. Hivyo wananchi wanasubiri kuona nini kitafanyika kutatua changamoto hii...kuna 'expectation gap' ambayo ni lazima izibwe ndipo watu wasadiki kushuhudia#‎MabadilikoYaKweli.