MAHAKAMA ZA ARDHI ZA KATA ZIJIREKEBISHE NA KUFANYA KAZI YAKE

MABARAZA ya adrhi ya kata yanadaiwa kuwa ni chanzo cha migogoro ya ardhi badaya ya kuwa ndio kimbilio na usuruhishi wa migogoro hiyo licha lengo la kuundwa kuwa ni utatuzi wa migogoro.

Hayo yanakuja baada ya baadhi ya wananchi akiwemo Prosper Mgaya, kuona mabaraza hayo hayana msaada kwao kutokana na utendaji kazi wake na kuona kuwa yamekuwa na rushwa nyingi na kuomba serikali kuyatengea fedha ili kuto penda hongo kutoka kwa wanaotaka hudumia.

Alisema kuwa mabaraza hayo yamekuwa yakiongeza migogoro badaya ya kupunguza na kuonekana ni bora kwenda mahakamani kuliko kwenda katika mabaraza hayo.

Uundwaji wa mabaraza hayo inahitaji kuwa na watu wasio pungua wanne na wasio zidi wanane na kuwa na uwiano sawa kati ya wanawake na wanaume na kutoa ruhusa ya mjume kutuma mwakilishi ila tu kwa wakili kuto mpa ruhusa ya kutuma mwakilishi wakati wa kusikiliza mashauri.

Aidha waliiomba mamlaka husika kuteua wajumbe wenye elimu ya sheria katika mabaraza hayo ili wasikilize mashauri ya ardhi kwa ufanisi mkubwa badala ya ubabaishaji unaofanywa na wajumbe wasiokuwa na uelewa wa sheria.

Mbunge wa Njombe Mjini Edward Mwalongo, aliahidi kushughulikia muundo wa mabaraza hayo kupitia madiwani kwa jimbo hilo ili yawe na ufanisi kwa jamii.

Alisema kuwa atahakikisha huwa mabaraza hayo yanakuwa msaada kama ilivyo tarajiwa na madhumuni ya kuundwa kwake.

“Kupitia madiwani wa kata za jimbo hili watayapitia mabaraza haya na kuyaunda upya ili kuondoa vitendo vinavyo waletea shida wananchi na kuhakikisha kuwa wananchi wanapata haki,” alisema Mwalongo

Mabaraza ya aridhi yameundwa hapa nchini chini ya sheria ya ardhi namba 2 ya mwaka 2002 kifungu cha 10 cha sheria hiyo pia inaelezea muundo wa mabaraza hayo pamoja na uwezo wake, mabaraza hayo yapo katika kila wilaya na yanauwezo wa kusuruhisha migogoro ya ardhi na mabaraza hayo yanatakiwa kutumia sheria ya ardhi ya mwaka 1999 na ile ya ardhi ya vijiji ya mwaka huohuo.