Chadema Njombe ; Tunaenda kuitaka mahakama itengue ushindi wa CCM jimbo Njombe Kusini

CHAMA cha demokrasia na maendeleo Chadema mkoa wa Njombe kimesema kuwa kimeanda ushahidi na nyaraka 14 tayari kwenda mahakamani kwaajili ya kuitaka mahakama kutengua matokeo ya ubunge jimbo la Njombe kusini ambalo alitangazwa mshindi kutoka chama cha CCM Edward Mwalongo.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutoka katika mkutano wa kuunda kamati ya kushugulkikia kesi hiyo aliye kuwa mgombea wa ubunge jimbo la Njombe Kusini Emanuel Masonga kupitia chama hicho alisema kuwa wamefanikiwa kukusanya nyaraka zikatazo enda kuwasaidia mahakamani.

Masonga alisema kuwa wamefanikiwa kukusanya ushadidi na nyalaka 14 ambazo chama cha mapinduzi CCM hakita kuwa na majibu, zitakazo wasaidia kuifanya mahakama itengue ushindi uliotangazwa na Tume ya uchaguzi kwa kumtangaza Mwalongo kuwa mshindi.

Alisema kuwa ushahidi wote wameshawakabidhi mawakili wao kwaajili ya kufungua kesi ambapo amesema kuwa kesi hiyo ambayo wanataraji kufungua mahakama kuu kanda ya Iringa itafunguliwa ndani ya wiki hii.

Alisema kuwa wakazi wa Jimbo lake la Njombe kusini wamejitolea kuhakikisha kuwa wanachangia gharama za kuendesha kesi hiyo itakapo anza mpaka itakapo fikia ukomo.

Alisema kuwa wanaenda mahakamani kupinga uteuzi aliouita ni batili uliotangazwa na Mkurugezi na kumtangaza yeye kuwa mshindi ama kuruduwa kwa uchaguzi katika jimbo hilo la Njimbe Kusini ili kutangazwa mshindi harali.

Alisema, wao kimsiongi wanaenda mahakamani kupinga kwa hoja ushindi wa Mwalongo,  huku akisema kuwa mahakama ndio itawaambia kuwa inakwenda kumtangaza mshindi upya au inakwenda kuufuta uchaguzi.

揘dugu waanduishi tuna hoja za msingi za kwenda kupinga maytokeo ambazo tutaziwasilisha mahakamani ambazo CCM na Mwalongo hawana majibu ya kuweza kuzipinga hoja hizo,� alisema Masonga na kuongeza,

"Sisi tunacho kwenda kuitaka mahakama ni kuondoa maamuzi ya kuwa Mwalongo ni mshindi, tuna nyaraka zisizo pungua 14 ziunazo onyesha Chadema imeshinda katika nafasi ya Ubunge katika jimbo hili, mahaka itaenda kuthibitisha kama itatenda haki katika suala letu,�aliongeza.

Hata hivyo Mwenyekiti wa kamati waliyounda kwaajili ya kushughulikia kesi hiyo Emmanuel Filangali alisema kuwa tayari vidhibiti vya kesi hiyo vimekusanywa na kupewa mawakili wao kwaajili ya kwenda kuisimamia kesi hiyo.

Kuhusu usajili wa kesi vilangali alisema kuwa wanatarajia kufungua kesi hiyo mwishoni mwa wiki hii au mapema wiki ijayo ili kuhakikisha ushindi walio pokwa wana lejeshewa na mahakama.

揔inacho subiliwa ni kwenda kusajili kesi mahakamani hiki ndicho watananzania wanatakiwa kuelewa ikisha sajiliwa tu tutawaambia tumepangiwa lini kuzanza kusikiliza kesi na ndicho tunacho kisubilia maana nyaraka zite tunazo tayari,� aliongeza Filangali.