Zimebaki siku kumi kuifikia October 25 2015 siku ambayo Watanzania watafanya maamuzi ya kuchagua Viongozi wao kwenye ngazi za Udiwani, Wabunge pamoja na Rais wa Jamhuri ya Muungano… stori zinazohusu Siasa ziko pia kwenye Headlines kila siku.
October 15 2015 baadhi ya Viongozi wa CHADEMA wamekaa Kikao na kujadili masuala makubwa mawili kuelekea siku ya Uchaguzi Mkuu 2015.
Kwanza ni hii kuhusu umbali ambao watu wanatakiwa kukaa baada ya kupiga kura >>> “Baada ya Wananchi kupiga kura, wasogee mita 200 wakae kulinda kura zao… Sio jambo la Kijinai,Sheria inaruhusu hivyo. Viongozi wanaoondoka Madarakani hawajui chochote kuhusiana na Sheria ya Uchaguzi” >>> John Mallya.
“Hivi Vituo vya Kupiga Kura haviko Mbinguni, kama ni Shule au Ofisi ya Kata ziko sehemu ya Makazi ya watu, sasa hao watu utawaambia nyumbani kwao waondoke siku hiyo?” >>> Hiki ndio alichokisema Mwanasheria wa CHADEMA, John Mallya.
Lakini kingine ilikuwa ni ishu ya Daftari la Wapigakura >>>> “Tumekuwa tukiiomba Tume ya Uchaguzi itoe Daftari, baada ya kushinikiza sana wametupa Daftari jana jioni.. Tumekuta matatizo baada ya kulipitia Daftari, katika Kituo kimoja tu kuna makosa zaidi ya 17.. ndani ya Daftari kuna Wachina wameandikishwa, kuna Godown, pikipiki vyote vimepigwa picha na kupewa Kadi za Kupigia Kura… Imekuwaje Tume imeshindwa kugundua tatizo hili, kwenye Picha nyingine za Vitambulisho watu wamejipiga selfie” >>> Reginald Munisi, Mkurugenzi Uchaguzi CHADEMA.
Hapa ni Pichaz zinazoonesha baadhi ya makosa ambayo wameyagundua kwenye Daftari la Wapigakura.