Wanafunzi njombe waishauri seikari kuhusu mabadiliko ya hali ya hewa

MWANAFUNZI wa shule za sekondari za Njombe Sekondari na Uwemba wameiomba serikali kusimamia sheria ya panda miti na kata miti kwa lengo la kupambana na mabadiliko ya hali ya hewa yanayo leta madhala mbalimbali duniani.

Wakizungumza baada ya kupatiwa elimu juu ya madhala ya mabadiliko ya hali ya hewa iliyo tolewa na mamlaka ya hali ya hewa Tanzania kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, waliwema kuwa ili kukabiliana na hali ya hewa ni lazima sheria ziwe na meno ili kupambana na mabadiliko hayo.

Mwanafunzi wa shule ya Uwemba Mkoani Njombe Salafina Jailo alisema kuwa serikali inatakiwa kuhakikisha kuwa kunautaratibu wa kuwabana wanao haribu mazingira bila  ya kurudishia uharibifu wake.

Alisema kuwa kuna sera ya panda miti kata mti haitekelezi kwa kuona watu wakikata miti na kuto panda mti kitu kinacho sababisha ardhi kupoteza uoto wa asili na kusababisha ongezeko la joto duniani.

“Kutokana na kuto kuwapo kwa utekelezeji wa sera ya udhibiti wa uharibifu wa mazingira serikali inaanza kupoteza vivutio vya utalii kama kuyeyuka kwa Barafu katika mlima kilimanjaro na kusababisha watalii kupungua na kuikosesha serikali mapato,” alisema Jailo.

Naye Festo Amanyisye mwanafunzi wa Uwemba, alisema kuwa ongezeko la joto na upungufu wa mvua hasa unasababisha na uharibifu wa mazingira unao tokana na ongezeko la viwanda na kuwa serikali inatakiwa kuchukua juhudi za makusudi kuielimisha jamii kuhusiana na utunzaji wa mazingira.

“Serikali inatakiwa kutekeleza sera ya Panda miti kata mti ili kurejesha hali ya hewa ya zamani na kuwa watu wanao kiuka sera hiyo kupewa adhabu ambayo itakuwa Mfano kwa wananchi wengine,” alisema Amanyisye.

Aidha Ngalaba Sospeter mwanafunzi wa shule ya sekondari ya Njombe (Njoss) ameitaka serikali kuongeza juhudi za kutoa elemu kwa umma hasa katika shule mbalimbali ili kuifikishia elimu kwa jamii kwa urahisi hasa madhara ya uharibifu ili kuibadilisha jamii.

Hata hivyo Frederick David mwanafunzi wa Njoss alisema kuwa kupitia elimu aliyo ipata kutoka kwa mamlaka ya hali ya hewa atakuwa barozi wa kuhakikisha anapambana na mabadiliko ya hali ya hewa ka kuhakikisha vitu vinavyo zuilika anashawishi kuvizuia.

Akizungumza baada ya kutoa elimu kwa wanafunzi wa shule hizo za Mkoani Njombe Mkurugenzi wa utafiti na matumizi ya hali ya hewa Tanzania Dr. Ladslaus Chang’a , alisema kuwa serikali kupitia mamlaka ya hali ya hewa imeanza kutoa elimu kuhusiana ana mabadiliko ya hali ya hewa ili kupambana na madhara yanayo jitokeza kila mwaka.

Alisema kuwa mabadiliko ya hali ya kewa yamekuwa yakisababisha kutokea kwa madhala mbalimbali kama mafuliko na kusababisha vifo, ukame na kusababisha vivyo vya wanyama huku elimu ikilenga upandaji wa miti na utunzaji wa mazingira.

 Alisema kuwa mamlaka hiyo imenzisha mfumo wa kutoa elimu na utabili wa hali ya hewa kwa njia za ujumbe mfupi kwa wananchi na wakulima wanao tegemeo kulima kwa kutumia utabili wa hali ya hewa hapa nchini.


Chang’a alisema kuwa elimu hiyo inatolewa kwa wanafunzi mashuleni kwa lengo la kuwajenga wakiwa bado mashuleni ili kuelemisha wazazi wao na kuwa na kizazi chenye elimu ya utunzaji wa mazingira.

Related Posts