Jinsi Teknolojia za Kisasa Zinavyoathiri Mahusiano ya Familia

madhara-ya-teknolojia-katika-familia-0

Maendeleo ya kiteknolojia ni muhimu kwa maendeleo ya jamii yoyote duniani. Tumeshuhudia haya katika nchi za Japan,China na nchi za Magharibi kama Marekani na Uingereza.

Lakini teknolojia hizi zina madhara pia katika jamii zetu na na kama kusipowekwa mipaka zinaweza kudhuru mahusiano baina ya wanafamilia.

Nitazungumzia madhara ya utumiaji wa TV,Simu za mikononi na intaneti,mitandao ya kijamii kama twitter,facebook,instagram na kubwa kuliko zote Whatsapp hali kadharika matumizi ya Kompyuta. Hizi ni teknolojia za kisasa zinazoingilia na kuharibu mawasiliano katika familia

Teknolojia za Kisasa 5 Zinazodhuru Ustawi wa Familia:

1. Televisheni na Video (TV)


madhara-ya-teknolojia-katika-familia-TV-chumbani
Nilikuwa na marafiki toka Ufaransa miaka kama kumi na mbili iliyopita,ukiwatembelea nyumbani kwao walikuwa wakizima TV,nilikuwa nikishangazwa sana na tabia hiyo. Nilipohoji waliniambia kuwa wanazima TV ili tuweze kuongea kwa uzuri zaidi.

TV inaingilia mawasiliano baina ya watu wanaotazama. Badala ya kuongea na kujadili mambo ya msingi baina yao TV inakuwa kikwazo.

Tunafanya makosa haya katika familia nyingi,mgeni akija basi atapewa rimoti za ving’amuzi vyote na deki ya video. Mazungumzo yanaishia kwenye kukaribishwa tu na watatumia muda mwingi kuangalia maisha ya watu wengine katika TV badala ya maisha yao.

Matumizi ya TV yanatakiwa kuangaliwa kwa ukaribu na kupunguza muda wa kuangalia.
Madhara ya TV kwa Watoto
TV kwa watoto inaelezwa kuwafanya wasijishughulishe na vitu vingine kama masomo na michezo na hivyo kudumaza akili zao na kutia uvivu miili yao. Watoto wanatakiwa kuangalia TV kwa ratiba na kwa programu maalumu tu ambazo zina maadili kwa watoto na zinazowasaidia kujifunza stadi za maisha.

2. Simu za Mkononi

madhara-ya-teknolojia-katika-familia-1
Simu za mikononi zimeleta mapinduzi makubwa katika kuboresha mawasiliano na zimechangia maendeleo ya kiuchumi na kijamii kwa kiwango kikubwa lakini pia zimeleta balaa kubwa katika kupotosha maadili na kuchngia ufisadi katika mahusiano ya familia hasa ya kimapenzi.

Simu zinachangia ugomvi mkubwa katika familia sasa hivi. Simu zinatumika kupanga mipango ya kiharifu na kifisadi.

Wapenzi wamekuwa wakitumia simu kupanga mipango ya udanganyifu katika mahusiano,japokuwa hii ni tabia ya mtu binafsi lakini teknolojia ya simu imerahisisha mambo haya kutokea kuleta vishawishi vikubwa.

Simu za Mkononi na Mtandao wa Intaneti
Mtandao wa intaneti katika simu na programu za kisasa za mawasiliano zimechochea moto mawasiliano baina ya watu. Urahisi huu wa kuwasiliana unatumika vibaya sasa hivi. Unapunguza sana mawasiliano ya ana kwa ana na badala yake watu wanapendelea zaidi kuwasiliana kwa simu.

Utakuta mtu yuko na mwenza wake nyumbani lakini kila mmoja yuko bize na simu yake akiwasiliana na wengine. Mawasilino ya ndani yanadhurumiwa na simu na mitandao ya kijamii.

Niliona picha moja ya vijana kadhaa waliamua kwenda kupata vinywaji pamoja lakini walipofika sehemu ya kinywaji wakaagiza kisha kila mmoja akageukia kwenye simu yake, hakuna mazungumzo tena yaliyoendelea. Hii ni hatari kubwa inayoletwa na teknolojia za kisasa katika jamii zetu.

3. Mitandao ya Kijamii

madhara-ya-teknolojia-katika-familia-mitandao-jamii
Nimeelezea kidogo juu ya madhara ya mitandao ya kijamii hapo juu lakini niongezee zaidi hapa. Mitandao ya kijamii inakata mawasilianio ya ana kwa ana. Watu wanapendelea zaidi kuwasiliana na watu walio mbali kuliko waliopo karibu nao. Whatsapp inaongoza katika madhara na ndiyo inayopendwa nakutumiwa na wengi.

Siku hizi ukienda katika sherehe za harusi mfano utaona katika meza nyingi watu wnashughulika na simu zaidi bila kujali tukio lililowaleta hapo. Maharusi wanabaki peke yao na MC.

Sehemu za kazi pia kumekumbwa na shida kubwa,mitandao ya kijamii katika simu inaingilia utengaji wa kazi. Na tatizo hili ni wazi litachangia kupungua kwa ufanisi na uzalishaji wa mashirika na makampuni mengi kama hakutachukuliwa hatua za haraka kudhibiti madhara ya teknolojia za kisasa.

4. Kompyuta

madhara-ya-teknolojia-katika-familia-2
Matumizi ya kompyuta hasa kompyuta mpakato kunaingilia mahusiano katika familia. Kwakuwa kompyuta hizi zinabebeka kirahisi watu wamekuwa wakihamisha kazi zao toka maofisini na kupeleka nyumbani.

Badala ya kushiriki na familia kama kucheza na watoto na kuongea na mwenza,utakuta mtu yuko bize na kompyuta. Hii inampa muda mdogo sana wa kuishi na familia yake. Kuna wanaohamishia kompyuta mpaka kitandani anapolala. Hii ni hatari kubwa kwa mahusiano.

Hatua za Kuchukuliwa Kudhibiti Hali

Kwa mawazo yangu,hatua za lazima na za makusudi zinatakiwa kuchukuliwa na kila mmoja katika kudhibiti madhara haya ya teknolojia za kisasa
  1. Wanajamii Kutambua Tatizo Kwanza

Kutambua kuwa kuna tatizo ni hatua moja ya kulitatua hivyo ni muhimu kwa kila mwanajamii na mwanafamilia kujua kuwa mitandao na teknolojia zinaleta madhara kama zikitumiwa vibaya na hivyo kujenga adabu ya matumizi yake.

Muda sahihi na sehemu sahihi kwa madhumuni maalumu uzingatiwe.
Amua kuzima simu kama unaenda kwenye sherehe kwa mfano, au acha kupokea ujumbe na kujibu kama ukiwa kazini au una mazungumzo na watu.
  1. Weka Utaratibu Maalumu wa Kutumia Simu na TV na Kompyuta

Jipangie uraratibu binafsi na familia yako. Mfano simu zisipokelewe wala ujumbe kujibiwa wakati wa kula.

Kuacha mawasiliano ya mitandao ya kijamii ukiwa na mwenza wako. Ikiwezekana kujitoa katika baadhi ya makundi yasiyo na tija labda kamani kundi la kifamilia na mnajadili mambo ya msingi.
Toa TV chumbani mnako lala, inaingilia mapenzi yenu.
Pangeni muda maalumu na vipindi vya kuangalia katika TV.
Amua kutotumia kompyuta nyumbani labda kwa kiasi kidogo ikibidi.

 Tuchukue Hatua Sasa

Matumizi ya teknolojia za mawasilioano zimeleta changamotyo katika maisha na mahusiano katika familia zetu na ni muhimu kuchukua hatua za kudhibiti.
Mabadiliko yanaanza na wewe hivyo chukua hatua sasa.