JESHI LA POLISI LAPIGA MARUFUKU ZIARA ZA KUSHTUKIZA MTAANI ZA LOWASSA!!,BAADA YA KUPANDA DALADALA,LEO LOWASSA AIBUKIA TANDIKA


Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, limepiga marufuku wagombea urais kufanya vitendo vinavyoweza kuhatarisha usalama wa wananchi.


Akiongea leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Kanda hiyo Suleiman Kova ametolea mfano kitendo cha jana cha mgombea urais wa Chadema Mhe. Edward Lowassa cha kufanya ziara ya kushtukiza kwa wananchi na kupanda daladala.


Amesema ziara hiyo ya Mhe. Lowassa na mgombea mwenza wake Juma Duni Haji walitembelea Gongo la Mboto, ingeweza kuhatarisha usalama wa wananchi kwa kuwa watu wengi walikusanyika na wengine kuacha kazi zao.



Wakati huo huo Mgombea wa Urais wa Ukawa Edward Lowassa pamoja na mgombea mwenza Juma Duni Haji leo wamewashitukiza wafanyabiashara katika soko la Tandika jijini Dar es salaam.


Aidha, wagombea hao waliwasili katika soko hilo asubuhi ya leo ambapo shughuli zilisimama kwa muda.

Kabla ya kuanza mazungumzo na wafanyabishara hao,Lowassa alikaribishwa chai na mmoja wa wafanyabiashara katika soko hilo.


Ziara hiyo ya kushitukiza iliyoanzia Mbagala siku ya jana ni maalumu kwa lengo la kuzungumza na wananchi wa hali ya chini kuhusiana na matatizo yanayowakumba katika maisha yao ya kila siku.