Serikali ya Kenya imeshindwa katika jaribio lake la kupinga uamuzi wa mahakama kuhusu sheria mpya ya usalama iliozua tetesi.
Mahakama ya rufaa imeunga mkono kutupiliwa mbali kwa baadhi ya vipengee kwenye sheria hiyo na mahakama ya chini hadi kesi ya kuipinga sheria hiyo iliowasilishwa na upinzani itakapoamuliwa.
Wanaoipinga sheria hiyo wanaitaja kuwa ya kukandimiza uhuru wa habari kwa kuruhusu mawasiliano kuzimwa bila amri ya mahakama na washukiwa kuzuiliwa hadi mwaka mmoja bila ya kufunguliwa mashtaka.
Mawaziri nchini Kenya wanasema kuwa sheria hiyo mpya itasaidia kupambana na wanamgambo wa al Shabaab.