Wahamiaji 107,000 waliwasili Ulaya Julai


Wahamiaji wamekuwa wakipoteza maisha baharini wanapokuwa safarini kuelekea Ulaya
Shirika la Umoja wa Ulaya linalopambana na maswala ya uhamiaji haramu na biashara ya binadamu, Frontex limetoa wito kwa nchi wanachama wa umoja huo kutoa msaada zaidi kwa nchi tatu zilizoathirika kutokana na kuwa na idadi kubwa ya wahamiaji.
Ugiriki, Italia na Hungary ni nchi zinazoelezwa kuathiriwa zaidi.
Shirika hilo limetaja hali hiyo kuwa ya dharula na kutoa wito wa kuongezwa kwa maofisa na vifaa zaidi ili kushughulikia tatizo hilo.
Frontex imesema mwezi uliopita zaidi ya Watu 107,000 waliwasili ulaya kwa njia za panya, ikiwa ni mara tatu zaidi ya waliowasili mwezi Julai mwaka jana.
Watu hao wengi wanaelezwa kutoka nchini Syria,Afghanistan na nchi za kusini mwa jangwa la Sahara wakikimbia hali mbaya ya usalama na umasikini