Waziri Mkuu wa Israel,Benjamin Netanyahu
Yair Lapid waziri wa Fedha wa Israel aliyefukuzwa kazi, ambaye ni mwenyekiti wa chama cha "Yesh Atid" kilicho katika serikali ya mseto ya Bwana Netanyahu
Waziri Mkuu wa Israel, Benjamin Netanyahu, ameiweka nchi katika hali ya kufanyika mapema uchaguzi wa bunge kwa kuwafukuza kazi mawaziri wawili waandamizi ambao ni viongozi wa vyama katika serikali yake ya mseto. Wakati wa mkutano na waandishi wa habari kupitia televisheni, Bwana Netayahu amewashutumu mawaziri wote wawili akiwemo waziri wa Fedha, Yair Lapid, na waziri wa Sheria, Tzipi Livni, kwa kupanga njama dhidi yake.
Wanasiasa wote wawili viongozi wa vyama vya mrengo wa kati, wamesema nchi imetumbukizwa katika uchaguzi usio wa lazima. Mwandishi wa BBC nchini Israel amesema Bwana Netanyahu huenda akataka utawala mpya utakaovihusisha vyama vya dini vinavyowakilisha madhehebu ya Wayahudi wa ultra-orthodox.