Rais wa Nigeria, Goodluck Jonathan, anafanya kampeni za uchaguzi katika mji wa kaskazini-mashariki mwa nchi wa Maiduguri.
Mji huo uko kati ya jimbo lilokumbwa na mashambulio mengi kabisa ya wapiganaji Waislamu, Boko Haram.
Ulinzi mkali umewekwa katika eneo la uwanja wa michezo ambako anahutubia wafuasi.
Kabla ya ziara ya rais, Boko Haram walishambulia kijiji nje ya Maiduguri na kuuwa watu kama 15.
Wadadisi wanamshutumu rais kuwa ameshindwa kuwalinda raia dhidi ya Boko Haram ambao wanadhibiti eneo kubwa la kaskazini-mashariki mwa Nigeria.