Obama aomba fedha kukabili Ebola

 

Rais Barack Obama wa Marekani
Rais wa Marekani Barack Obama ametoa wito kwa chama cha Congress kupitisha kiasi cha dola bilion 6 kwa lengo la kukabiliana na mlipuko wa ugonjwa hatari wa Ebola katika nchi za Afrika Magharibi.
Obama amesema hayo muda mfupi baada ya kutembelea taasisi ya taifa afya nchini humo,ambapo aliwapongeza madaktari na wanasayanzi kwa kazi nzuri wanayoifanya kukabiliana na ugonjwa huo.
Mazishi wagonjwa wa Ebola
Inakadiriwa kuwa takriban watu 7,000 wamekufa kutokana na ugonjwa wa Ebola katika nchi za Liberia, Sierra Leone na Guinea.
Chama cha madaktari wasio na mipaka Medecins Sans Frontieres (MSF) kwa mara nyingine imelaumu taasisi za kimataifa kwa madai kuwa bado hawajaonyesha jitihada zao.
It described it as patchy and slow, with the job of tackling the crisis largely left to doctors, nurses and charity organisations.
MS katika ripoti yake imesema serikali za kigeni kama vile Uingereza zimeendelea kujenga vituo vya matibabu ya ugonjwa huo.
Jumanne wiki hii shirikisho la chama cha Msalaba Mwekundu limesema kuna unyanyapaa dhidi ya watu wanaotoka katika nchi zilizokumbwa na ugonjwa huo.