YALIOJIRI DODOMA LEO BUNGE LA KATIBA.

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akipiga kura leo kwenye ukumbi wa Bunge Maalum la Katiba mjini Dodoma kupitisha Sura na Ibara za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Yahya Kassim Issa akiomba mwongozo leo Bungeni kwa Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta kuhusu kitendo cha Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman kuja kupiga kura na kukataa baadhi ya Ibara za Rasimu ya Katiba inayopendekezwa wakati alijitoa kwenye Kamati ya Uandishi ambapo alitakiwa awepo akitetea maslahi ya Zanzibar, jambo ambalo limewachanganya baadhi ya wajumbe. 
Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman akisindikizwa kutoka ndani ya ukumbi wa Bunge Maalum leo mjini Dodoma na Askari Polisi.

Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othman (mwenye Kaunda suti ya kijivu) akisindikizwa kutoka nje ya viwanja vya Bunge Maalum la Katiba leo mjini Dodoma na Askari Polisi mara baada ya kushutumiwa na baadhi ya Wajumbe wa Zanzibar. 
Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mzee Kingunge Ngombale Mwiru pamoja Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wakibadilishana mawazo kwenye viwanja vya bunge hilo mjini Dodoma leo. 
Waziri Mkuu wa Tanzania ambaye pia ni mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Mizengo Pinda akibadilishana mawazo kwenye viwanja vya bunge hilo mjini Dodoma leo na Mjumbe Wabunge hilo nje jengo la bunge Dodoma.(Picha na Benedict Liwenga, Maelezo-Dodoma)