Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho kilifungwa kutokana na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji.
Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameahidi kulitafutia ufumbuzi tatizo la wakulima wa chai katika Jimbo la Bumbuli ndani ya mwezi mmoja ujao. Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho kilifungwa kutokana na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji. Kinana aliwalaumu viongozi wa Serikali ya mkoa kutumia muda mrefu kushughulikia matatizo ya wakulima na kutolea mfano tatizo la kiwanda hicho lililoanza mwaka 2008. “Mgogoro huu ni wa siku nyingi, watu wanatupiana mpira tu...Badala ya kuchukua hatua kuutatua, wao wanaleta porojo. Viongozi wa Serikali wanawapuuza wakulima wakati wao mambo yao yako safi,” alisema. Kinana aliwaambia wananchi hao kuwa atalifikisha suala hilo katika Kamati Kuu ya CCM inayohudhuriwa na viongozi wote wa juu nchini. “Tutakwenda kujifungia na kuulizana maswali magumu... ni lazima walioshindwa kulishughulikia suala hili wawajibike, kama hawataki kuwajibika kwa hiari basi wawajibishwe,” alisema. Alibainisha kuwa kumekuwa na kulindana ndani ya Serikali na ndio maana viongozi wanaoshindwa kushughulikia matatizo ya wananchi wanaendelea na utumishi bila ya kuchukuliwa hatua zozote kwa haraka. Awali, wananchi waliohudhuria mkutano huo walimtimua diwani wao, Richard Mbuguni ambaye walimtuhumu kushirikiana na mwekezaji huyo kuwadhulumu wakulima. Wananchi hao walifanya hivyo baada ya mwenyekiti wa wakulima wadogo wa chai katika eneo hilo, Almas Shamshama kumtaka kiongozi huyo kuondoka katika mkutano huo.Kinana aahidi kusaidia wakulima Mponde SHARE BOOKMARKPRINTEMAILRATING Na Rais Said, Mwananchi Posted Jumatano,Oktoba1 2014 saa 8:14 AM KWA UFUPI Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho kilifungwa kutokana na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji. SHARE THIS STORY 0 inShare Bumbuli. Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana ameahidi kulitafutia ufumbuzi tatizo la wakulima wa chai katika Jimbo la Bumbuli ndani ya mwezi mmoja ujao. Alitoa ahadi hiyo juzi jioni alipohutubia mkutano wa hadhara katika eneo la Mponde, karibu na kiwanda cha chai ambacho kilifungwa kutokana na mgogoro kati ya wakulima na mwekezaji. Kinana aliwalaumu viongozi wa Serikali ya mkoa kutumia muda mrefu kushughulikia matatizo ya wakulima na kutolea mfano tatizo la kiwanda hicho lililoanza mwaka 2008. “Mgogoro huu ni wa siku nyingi, watu wanatupiana mpira tu...Badala ya kuchukua hatua kuutatua, wao wanaleta porojo. Viongozi wa Serikali wanawapuuza wakulima wakati wao mambo yao yako safi,” alisema. Kinana aliwaambia wananchi hao kuwa atalifikisha suala hilo katika Kamati Kuu ya CCM inayohudhuriwa na viongozi wote wa juu nchini. “Tutakwenda kujifungia na kuulizana maswali magumu... ni lazima walioshindwa kulishughulikia suala hili wawajibike, kama hawataki kuwajibika kwa hiari basi wawajibishwe,” alisema. Alibainisha kuwa kumekuwa na kulindana ndani ya Serikali na ndio maana viongozi wanaoshindwa kushughulikia matatizo ya wananchi wanaendelea na utumishi bila ya kuchukuliwa hatua zozote kwa haraka. Awali, wananchi waliohudhuria mkutano huo walimtimua diwani wao, Richard Mbuguni ambaye walimtuhumu kushirikiana na mwekezaji huyo kuwadhulumu wakulima. Wananchi hao walifanya hivyo baada ya mwenyekiti wa wakulima wadogo wa chai katika eneo hilo, Almas Shamshama kumtaka kiongozi huyo kuondoka katika mkutano huo.
Na Mwananchi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)