Tofauti ya kidini yavunja ndoa India

Ndoa ya kihindi
Maafisa wa polisi katikati mwa India wamefutilia mbali harusi kati ya mwanamume mkristo na mwanamke wa kihindu baada ya shinikizo kutoka kwa makundi ya kihindu yenye mrengo wa kulia.
Wanandoa hao wawili kutoka Madhya Pradesh walitoroshana na kuoana katika sherehe ya kihindu bila ruhusa ya familia ya msichana.
Baada ya makundi hayo ya Kihindu kupinga hatua hiyo na kutishia kushambulia majengo ya serikali,maafisa wa polisi katika eneo hilo waliwasaka wapenzi hao na kuwalazimisha kuachana.
Waandishi wanasema kuwa hatua hiyo ya makundi ya kihindu imekuwa ya kawaida katika jimbo hilo katika siku za hivi karibuni.