Messi matatani kwa kukwepa kodi

Lionel Messi
Nyota wa timu ya Barcelona na Argentina Lionel Messi anakabiliwa na mashtaka ya ukwepaji wa kodi,hii ni kwa mujibu wa jaji mmoja wa Uhispania.
Jaji huyo amepinga ombi la kiongozi wa mashtaka la kufutilia mbali mashtaka hayo kwa madai kwamba babake mchezaji huyo ndiye anayesimamia fedha zake.
Messi na babaake Jorge wanashtakiwa kwa kuiibia mamlaka ya taifa hilo zaidi ya yuro millioni 4.
Wote wamekana kufanya makosa hayo yalioanza mwaka 2007.