WAFANYA BIASHARA ndogondogo maarufu (Machinga) jijini Mbeya, wanaomba kukutana na Rais wa Jamuhuri ya Muungano
wa Tanzania, Jakaya Kikwete, atakapo wasili jijini Mbeya kuadhimisha miaka 37
ya kuzaliwa kwa chama cha mapinduzi (CCM), ili waweze kumtolea kero zao.
Akizungumza na Elimtaa Blog jijini Mbeya mmoja viongozi wa
machinga aitwae Dickson Kalapila alisema kuwa, wamekuwa wakipata shida kuhusu
maeneo ya kuuzia bidhaa zao kuanzi mwaka 2011 kutokana na ufinyu wa maeneo ya
kufanyia biashara.
Alisema walifikisha kiliochao kwa viongozi wa halmashauri ya
jiji la mbeya ili wawapatie sehemu ya kufanyia kazi, ambapo walionyeshwa maeneo
ya Mwanjelwa nyuma ya soko jipya linalo jengwa.
Kalapila alisema baada ya hapo hakuna jambo lolote linalo
endelea, hali ambayo inazidi kuwapa wasiwasi mkubwa.
Nae wenyekiti wa machinga katika eneo la Kabwe James Mwepa
alisema walipewa eneo la kufanyia kazi katika barabara ya kwanza iendayo Block
T kuzunguka gereza la watoto watukutu na kwamba stendi ya mabasi ya mzunguko
(daladala) yaendayo mbalizi na Uyole yangehamishiwa pale aliongeza kuwa
chakushangaza ni kwamba hadi kufikia leo hakuna dalili za kujengwa kwa stendi
hiyo japokuwa vibanda vipo, na kwamba katika lile eneo bila stendi eneo hilo
sio rafiki kwa biashara.
Alisema baada ya kuona kimya kimezidi yeye pamoja na viongozi
wenzake walimfuata mkurugenzi wa jiji la Mbeya wawakati huo Juma Iddy, na
kumueleza shida zao ambapo aliwajibu kuwa waanze kufanya shughuli zao na ndipo
huduma zitafuata.
Mwepa alisema kuwa walishindwa kufanya biashara zao kwa
sababu ya kukosa huduma za msingi kama vile vyoo maji na barabara.
Alisema hata hivyo kiongozi huyo alisema kuwa mpaka sasa
huduma za barabara na maji zipo isipokuwa vyoo, ambavyo havieleweki vitajengwa
lini.
Ombi kubwa la wamachinga hao kwa Rais ni kutaka wajengewe
kituo kipya cha stendi ya jiji katika eneo lililopo gereza la watoto watukutu
kabla ya kuhamia eneo hilo kwa kuwa ni kubwa na lipo katikati ya mji.
Alimalizia kwa kusema kuwa kwa kufanya hivyo jiji litakuwa
limemaliza tatizo la wamachinga, na msongamano wa magari unaoendelea kuwepo
siku hadi siku kutoka Soweto, Kabwe mpaka mafiati.
Juhudi zao za kukutana na Rais zimekwama baada ya kumtuma
mwakilishi wao, filimon Mwansasu ili kutafuta upenyo wa kuonana na kutoa shida
zao zimekwama.