MAFUNZO YA KUPAMBANA NA UKATILI WA KIJINSIA YATOLEWA NA JESHI LA POLISI

 

 

photo 
Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro, kamishna msaidizi mwandamizi wa Polisi (SACP) Faustine Shilogile, wapili kutoka kushoto waliokaa, akifuatiwa na Naibu kamishna wa Polisi (DCP) Adolfina Chialo, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa semina ya mafunzo ya siku tano ya namna ya kupambana na makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto yanayofanyika mkoani Morogoro.(picha na Demetrius Njimbwi, Jeshi la Polisi)
………………………………………………………

Jeshi la Polisi nchini limesema kuwa, maendeleo ya nchi yeyote duniani yanategemewa kwa kiasi kikubwa na uwekezaji katika elimu na ulinzi wa mtoto, dhidi ya aina zote za unyanyasaji katika ngazi ya familia pamoja na jamii inayomzunguka.
Akizungumza na waandishi wa habari pamoja na washiriki wa mafunzo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku tano yanayofanyika mkoani hapa ya namna ya kushughulikia makosa ya ukatili wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto,  Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro,  (SACP), Faustine Shilogile, amesema kuwa, kwa sasa kumekuwa na taarifa nyingi zinazotolewa katika vituo vya Polisi kote nchini, taarifa ambazo nyingi zikihusisha watu mbalimbali kufanyiwa vitendo vya kikatili.
Pamoja na kudharirishwa  kijinsia ambapo kamanda Shilogile, amesema kuwa,  jamii inatakiwa kuhakikisha ulinzi na usalama wa mtoto kwa kuepuka vitendo vya uvunjifu wa amani hususan aina zote za  ukatili wa majumbani, jambo ambalo litaongeza tija katika maendeleo, alisema.
Aidha, kamanda Shilogile, amesema kuwa, kupitia mafunzo haya kwa askari wa Dawati la jinsia na watoto kuhusu kushughulikia makosa yanayohusu ukatili ambapo itasaidia kuongeza ujuzi na kubadilishana uzoefu na kuongeza ufanisi kwa askari Polisi katika kushughulikia makosa yanayohusiana na ukatili wa kijinsia, alisema.
Hata hivyo, Mkuu wa Dawati la jinsia na watoto Nchini, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP) Adolfina Chialo, amesema kuwa, licha ya Jeshi la Polisi kuwa na jukumu la kuhakikisha usalama wa raia na mali zao, hivyo dawati la jinsia linawajibu wa kuhakikisha linatoa huduma bora kwa jamii, alisema.
Kamanda Chialo, ameongeza kuwa, kutokana na mafunzo haya kutolewa kwa watendaji wa jeshi la Polisi na kuwahusisha washiriki kutoka katika kanda tatu za mikoa ya Dodoma, Pwani pamoja na Morogoro,  na kudhaminiwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), yatasaidia zaidi katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia na kuifanya jamii kutokuwa na takwimu za matukio ya ukatili wa kijinsia.
Na Kamanda wa Matukio