Habari
zilizopatikana zinasema kuwa Daraja la Dumila lililopo mkoani Morogoro
ambalo ni barabara ya Dodoma – Morogoro limekatika na magari hayapiti
baada ya mvua kubwa kunyesha usiku wa kuamkia leo.
Baadhi
ya magari yatokayo upande wa Dodoma na Morogoro yameamua kugeuza na
kurudi yalipotokea maana hakuna njia nyingine zaidi ya hiyo.
Kutokana
na mvua hiyo madarasa katika Shule ya Msingi Magole, Dumila, Morogoro
nayo yamefunikwa na maji na wanafunzi kuamua kujiokoa kwa kupita
madirishani. Mpaka sasa hali bado si nzuri eneo hilo la Dumila wilayani
Mvomero
Na Pamoja Blog