Utalii Online: KARIBU MBEYA KWA UTALII WA DARAJA ZURI ZA ASILI


Karibu Mbeya ujionee daraja la Mungu wilayani RungweNajua umewahi ona madaraja ya kila kabila, lakini umewahi kufikiria juu ya daraja lililojitengeneza lenyewe? Linaitwa Daraja La Mungu. Lipo Kiwira wilayani Rungwe huko Mbeya. Hapa maji ya Mto Kiwira yakiwa safarini kuelekea Ziwa Nyasa yalipasua mwamba na kuufanya uunde daraja ambalo watu hupita juu yake.
Unaweza ukawa umeona maajabu mengi. Kama hujafika hapa basi umesahau jambo muhimu sana.
#UzuriwaTanzania